Rais Dkt.Mwinyi awataja wanaokumbana na utumbuaji baada ya kuwaumiza wananchi muda mrefu

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Hussein Ali Mwinyi amewataka wananchi kuondoa shaka katika utaratibu wa kutumbua kwani wanaotummbuliwa ni wale wanaotumia fedha za umma kwa maslahi yao binafsi, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Rais Dkt.Mwinyi akiwahutubia wanachama na wananchi baada ya kuzindua tawi hilo.

Rais Dkt. Hussein Mwinyi ameyasema hayo leo Januari 5, 2021 mara baada ya kulifungua Tawi la Chama Cha Mapinduzi (CCM) la Matale, lililopo Jimbo la Chonga, Mkoa wa Kusini Pemba.

Amwsema kuwa, kinachotakiwa ni fedha za umma kutumika kwa mambo ya umma kwani kuna changamoto nyingi nchini zikiwemo maji, afya na nyinginezo kwa hivyo, wasiposhughulikiwa wabadhirifu na wezi maendeleo hayatapatikana.

Rais Dkt. Mwinyi amesisitiza kuwa, kusudi lake ni kuweka nidhamu katika matumizi ya fedha za umma ili kuleta maendeleo na kuwapongeza wana CCM na wananchi kwa mwitikio wao kwa kuunga mkono juhudi za maendeleo zinazochukuliwa hivi sasa.
Tawi la Mtale ambalo limejengwa kisasa ambalo leo Rais Dkt.Hussein Ali Mwinyi amelizindua rasmi.

Amewapongeza wana CCM kwa ushindi mkubwa wa kishindo uliopatikana katika uchaguzi mkuu uliopita na kuwapongeza wanaCCM wa Matale kwa kujenga tawi hilo la kisasa na kueleza jinsi alivyofarajika na ujenzi huo.

Aidha, amewapongeza wale wote waliochangia ujenzi wa tawi hilo na kumpongeza Khamis Yussuf Matale kwa ufadhili wa ujenzi wa tawi hilo pamoja na wanachama wengine wa CCM.

Post a Comment

0 Comments