Rais Dkt.Mwinyi:Usalama na hali nzuri kwa wananchi ndiyo lengo kubwa la Serikali

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema kuwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa imeundwa kwa lengo la kuendeleza na kudumisha amani, umoja na mshikamano miongoni mwa wananchi wa Zanzibar, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi akihutubia katika ufunguzi wa mkutano wa Kongamano la Pili la Amani Zanzibar lililoandaliwa na Friends of Zanzibar, lililofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Zanzibar Beach Resort jijini Zanzibar, kulia kwa Rais ni Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Mheshimiwa Zuberi Ali Maulid, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Sheria,Katiba Utumishi na Utawala Bora Zanzibar, Mheshimiwa Haroun Ali Suleiman.(Picha na Ikulu/Diramakini).

Mheshimiwa Rais Dkt.Hussein Ali Mwinyi ameyasema hayo Januari 16, 2021 katika hotuba yake ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Pili wa Amani uliofanyika huko katika ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Beach Resort, Mazizini nje kidogo mwa Jiji la Zanzibar. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt. Hussein Ali Mwinyi akizindua Kalenda ya Amani Milele, wakati wa hafla ya ufunguzi wa Kongamano la Pili la Amani lililofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Zanzibar na (kulia kwa Rais) Mwakilishi wa Waandishi waliopata Elimu ya Amani, Ndg.Abubakar Harith na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Sheria Katiba Utumishi na Utawala Bora Zanzibar, Mhe. Haroun Ali Suleiman.(Picha na Ikulu,Diramakini). Katika maelezo yake, Rais Dkt. Mwinyi amesema kuwa, mkutano huo umefanyika wakati mwafaka ambapo nchi imefanikiwa kufanya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 katika hali ya amani na ulivu mkubwa. 

Amesema kwamba, suala la kuendeleza na kudumisha amani hapa Zanzibar limepewa kipaumbele katika Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 pamoja na mipango ya maendeleo ya Kitaifa. 

Akinukuu Katiba hiyo katika kifungu cha 9(2-b) kimeeleza kwamba “Usalama na hali nzuri kwa wananchi itakuwa ndiyo lengo kubwa la Serikali”. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akionesha Kalenda ya Amani Milele baada ya kuizindua katika hafla ya Ufunguzi wa Mkutano wa Kongamano la Pili la Amani lililofanyika katika ukumbi wa Zanzibar Beach Resort na kulia kwa Rais ni Mwakilishi wa Waandishi wa habari waliopata mafunzo ya Amani, Ndg.Abubakar Harith na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Sheria Katiba Utumishi na Utawala Bora Zanzibar, Mhe.Haroun Ali Suleiman.(Picha na Ikulu/Diramakini). Mufti Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Sheikh Abdalla Luamba Mangara akitoa Salamu za Friends of Zanzibar wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Kongamano la Pili la Amani Zanzibar uliofanyika katiuka ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu).

Rais Dkt.Mwinyi ameongeza kuwa, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Awamu ya Nane itaendelea kufanya kila linalowezekana kwa ajili ya kuendeleza fikra za waasisi wa nchi hii na viongozi waliotangulia katika kudumisha umoja na mshikamano wa wananchi wa Zanzibar. 

Ameongeza kuwa, ni ukweli usio na shaka kwamba maendeleo hayawezi kupatikana katika nchi yoyote bila ya kuwepo amani na mshikamano. 

Kwa msingi huo, Dkt.Mwinyi amewahimiza viongozi wa vyama na Serikali, viongozi wa dini na madhehebu mbalimbali, vyombo vya habari, wazee na vijana katika jamii kushirikiana katika kudumisha misingi muhimu ya amani ili hali ya amani iliyopo hapa Zanzibar izidi na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania izidi kuimarika.
Viongozi wa Serikali wakifuatilia ufunguzi wa Mkutano wa Kongamano la Pili la Amani Zanzibar, wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akilihutubia na kulifungua katika ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini wa kwanza ni Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Mhandisi Zena Ahmed Said, Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Dkt. Mwinyi Talib Haji, Naibu Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Mahmoud Mussa na Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar, Sheikh. Hassan Othman. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Balozi wa Norway nchini Tanzania, Mhe.Elisabeth Jacobsen (hayupo pichani) akitoa salamu wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Kongamano la Amani Zanzibar lililofanyika katika ukumbi wa Zanzibar Beach Resort Zanzibar na kuandaliwa na Friends of Zanzibar.(Picha na Ikulu/Diramakini).

Aidha, Rais Dkt. Mwinyi amesisitiza haja ya kushirikiana na nchi za jirani katika Bara la Afrika katika kulinda hali ya amani na utulivu. 

Rais Dkt. Mwinyi amesisitiza haja ya kushikamana katika kuhubiri amani na utulivu katika nyumba za ibada, taasisi za Serikali na ndani ya jamii na familia huku akieleza haja kwa vyombo vya habari kuendelea kuwa makini ili kujiepusha kusambaza habari zinazoweza kuhatarisha amani. 

“Sote tuwe tayari kushirikiana katika kurejesha amani pale ilipotoweka,"amesema Rais Dkt.Hussein Ali Mwinyi. 

Sambamba na hayo, Rais Dkt.Mwinyi ameeleza kutodharau mambo madogo madogo yanayoweza kuhatarisha amani, kwani amani inapotoweka ni tabu kuirejesha na kujifunza kwa wale waliopata mitihani ya kuondolewa amani na utulivu. (Picha na Ikulu/Diramakini). Balozi wa Norway nchini Tanzania, Mhe.Elisabeth Jacobsen akitoa salamu za nchi yake wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Kongamano la Pili la Amani Zanzibar lililoandaliwa na Friends of Zanzibar katika ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu/Diramakini).Rais Dkt.Mwinyi alitoa pongezi zake kwa Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Katiba, Sheria Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa kushirikiana na Ofisi ya Mufti pamoja na Taasisi ya Marafiki wa Zanzibar (Friends of Zanzibar) kwa kuandaa mkutano huo. 

Dkt. Mwinyi aliwakaribisha wageni wote waliokuja katika mkutano huo na kuwahimiza kutembelea vivutio vya utalii ili wajifunze historia na utamaduni wa watu wa Zanzibar kwani yamo mambo mengi ya kujifunza kuhusu amani katika historia na utamaduni wa Kizanzibari. 

Amewataka washiriki wa mkutano huo kutoa michango yao na uzoefu walionao katika kulinda amani kwa kutegemea uzoefu na taaluma zao na kueleza imani yake kwamba maazimio yatayopitishwa katika mkutano huo yatakuwa na mchango mkubwa katika juhudi za kulinda na kudumisha hali ya amani. 

Nae Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad akitoa salamu zake katika mkutano huo amesema kuwa suala la amani si suala la hiari kwani bila ya amani hakuna maendeleo na pia, amani ni msingi wa kila kitu. 

Maalim Seif ameeleza kwamba maridhiano yanahitaji kulelewa ili vizazi vijavyo viweze kuja kurithi. 

Makamu wa Pili Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdulla na yeye kwa upande wake ametoa pongezi kwa waandaaji wote wa Mkutano huo na kusisitiza kwamba amani ni msingi wa maendeleo huku akieleza haja ya kuengezwa washiriki katika mkutano ujao kutokana na umuhimu wa mkutano huo. 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Haroun Ali Suleiman amezipongeza juhudi za Rais Dkt.Mwinyi katika kuitunza amani iliyopo huku akiwataka wananchi waendelee kuunga mkono juhudi hizo ili amani izidi kudumu. 

Mapema Mabalozi wa nchi za Jumuiya ya Ulaya zikiwemo Ujerumani, Norway na Switzerland kwa nyakati tofauti wamepongeza hatua za makusudi zilizochukuliwa na Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Mwinyi pamoja na Maalim Seif Sharif Hamad za kuwa na ushirikiano wa pamoja katika kuidumisha amani na hatimae kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa. 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Sheria Katiba Utumishi na Utawala Bora Zanzibar, Mhe. Haroun Ali Suleiman akizungumza wakati wa hafla ya ufunguzi wa Mkutano wa Kongamano la Pili la Amani Zanzibar lililoandaliwa na Friends of Zanzibar katika ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu/Diramakini).Wajumbe wa Mkutano wa Kongamano la Pili la Amani Zanzibar lililoandaliwa na Friends of Zanzibar, wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dkt.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) lililofanyika katika ukumbi wa Zanzibar Beach Resort jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu/Diramakini).

Mabalozi hao wameeleza matarajio yao makubwa kwa Zanzibar na kusisitiza kwamba wataendelea kuiunga mkono katika kuhakikisha amani iliyopo inadumishwa sambamba na kuendeleza kushirikiana na Zanzibar katika masuala mbalimbali ya maendeleo. 

Mapema wawakilishi wa Taasisi ya Marafiki wa Zanzibar (Friends of Zanzibar) kutoka Msumbiji, Malawi, Congo DRC, Rwanda, Burundi, Kenya na Tanzania Bara kwa nyakati tofauti walitoa salamu zao ambazo ziliwapongeza viongozi na wananchi wa Zanzibar kwa kuimarisha amani, umoja na mshikamano. 

Viongozi hao walimpongeza Rais Dkt. Mwinyi kwa kuonesha uongozi bora na uliotukuka hatua ambayo imeweza kudumisha Serikali ya Umoja wa Kitaifa huku wakimpongeza Maalim Seif Sharif Hamad kwa kukubali kuwa miongoni wa viongozi wa Serikali hiyo. 

Walieleza matumaini yao makubwa kwa Zanzibar ambapo waliitabiri kuwa ni sehemu itakayopata maendeleo makubwa na ya haraka kutokana na kuwepo kwa amani, umoja na mshikamano huku na wao wakiahidi kuendelea kuiunga mkono. 

Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabih amewakaribisha wageni wote kutoka nje ya Zanzibar katika mkutano huo huku akieleza umuhimu wa amani. 

Mkutano huo wa Amani umeshawahi kufanyika hapa Zanzibar na huo wa leo utakuwa ni wa pili ambapo ule wa mwanzo ulifanyika hapa Zanzibar mnamo mwaka 2015 kabla ya Uchaguzi Mkuu. 

Viongozi mbalimbali wamehudhuria kutoka ndani na nje ya Zanzibar katika mkutano huo wa siku mbili ambapo moja kati ya mada zitakazowasilishwa ni “Mambo tunayopaswa kujifunza baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe na mauaji yaliyotokea nchini Rwanda”. 

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news