TAMWA-Zanzibar yampongeza Mkurugenzi wao kwa tuzo

Chama cha waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA-Zanzibar) Zanzibar kimempongeza Mkurugenzi wao, Dkt.Mzuri Issa kwa kupata tunzo ya kutoa mchango mkubwa katika jamii kwenye maisha yake, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Tunzo hiyo imetolewa na waandaaji wa Tunzo za Vijana Zanzibar (ZYA) hii ikiwa ni mara ya pili mfululizo.

Mkuu wa jopo la majaji, Bw. Rashid Mohammed Rashid amesema, mara hii pamoja na kuitoa zawadi kwa vijana wameona pia watoe tunzo kwa watu waliosaidia sana maendeleo ya vijana nchini.

Wengine wanne waliopewa tunzo hizo ni Daudi Kombo Maalim, Shaib Ibrahim Mohamed, Raza Lee na DJ Saleh katika hafla iliyohudhuriwa na Waziri wa Habari, Vijana, Mh Tabia Mwita huko Michenzani Mall jana usiku.

Dr. Mzuri amepata tunzo hiyo kutokana na kuwawezesha vijana wanawake katika nyanja mbalimbali za kimaendeleo.

Post a Comment

0 Comments