TANGAZO LA NAFASI YA KAZI YA KATIBU MUHTASI


Shirika la Habari la Kanisa la Waadventista wa Sabato Tanzania (TAMC)

linalosimamia Hope Channel Tanzania, Morning Star Radio, Adventist World

Radio, Gazeti la Sauti Kuu na Voice of Prophecy linatangaza Nafasi ya Kazi

ya Katibu Muhtasi.

Sifa za mwombaji:

1. Mwombaji awe ni Mtanzania

2. Awe amehitimu kidato cha nne

3. Awe amehudhuria mafunzo ya uhazili na kufaulu

4. Awe amefaulu somo la Hatimkato ya Kiswahili na Kingereza kwa maneno 80 kwa dakika moja.

5. Awe mchapakazi, mwadilifu na mwenye uwezo wa kutumika katika

Nyanja mbalimbali za taaluma yake

Maombi yatumwe kwa Ofisi ya Mkurugenzi, Tanzania Adventist Media Channels, P.O. Box 77170, Dar es salaam, au yafikishwe moja kwa moja katika ofisi za Tanzania Adventist Media Channels, zilizopo Mikocheni B, jijini

Dar es salaam. Kwa walio nje ya Dar es salaam watume maombi kwa anuani yetu ya barua pepe ya writetotamc@gmail.com au info@morningstartv.or.tz

Barua ya maombi imbatanishwe na Wasifu Binafsi (CV), Barua ya ushuhuda toka kwa Kiongozi wa Kiroho, pamoja na vyeti vya Taaluma.

Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 26/01/2021 na usaili wa kwanza utakaombatana na mchujo utafanyika tarehe 27/01/2021 kwa wote waliotuma maombi. Ukisikia tangazo hili mjulishe na mwenzako.

KUMBUKA: Sharti la kufika kwenye usaili wa tarehe 27/01/2021 ni kutuma maombi.

Kwa maelezo zaidi piga 0765 154 752

Post a Comment

0 Comments