Utabiri wa hali ya hewa/ Weather Forecast today January 19, 2021

Utabiri wa hali ya hewa wa saa 24 zijazo kuanzia saa 3 usiku wa leo Januari 19, 2021 unaletwa kwenu na mchambuzi Noel Mlay kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA).

WEATHER FORECAST JANUARY 19th, 2021
Weather forecast for the next 24 hours starting 21:00 tonight on today January 19, 2021 as presented by analyst Thereza Ngassa from Tanzania Meteorological Authority (TMA).


UTABIRI WA HALI YA HEWA KWA SAA 24 ZIJAZO KUANZIA SAA 3.00 USIKU WA LEO: TAREHE: 19/01/2021..

....................................................................

Mikoa ya Lindi, Mtwara, Iringa, Njombe, Songwe, Mbeya, Rukwa, Kigoma, Tabora, Katavi, Dodoma na Singida inatarajiwa kuwa na Hali ya mawingu, mvua na ngurumo katika maeneo machache na vipindi vifupi vya jua.

.....

Mikoa ya Kagera, Geita, Mwanza, Shinyanga, Mara, Simiyu, Ruvuma na Morogoro inatarajiwa kuwa na Hali ya mawingu kiasi, mvua na ngurumo katika maeneo machache na vipindi vya jua.

.....

Mikoa ya Kilimanjaro, Manyara na Arusha inatarajiwa kuwa na Hali ya mawingu kiasi, mvua katika maeneo machache na vipindi vya jua.

.....

Mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, Pwani (ikijumuisha Visiwa vya Mafia) pamoja na Visiwa vya Unguja na Pemba inatarajiwa kuwa na Hali ya mawingu kiasi, mvua nyepesi katika maeneo machache na vipindi vya jua.

.....

ANGALIZO

VIPINDI VIFUPI VYA MVUA KUBWA VINATARAJIWA KATIKA BAADHI YA MAENEO YA MIKOA YA MTWARA, LINDI, RUVUMA, KUSINI MWA MKOA WA MOROGORO, IRINGA NA NJOMBE.

.....

VIWANGO VYA JOTO KWA BAADHI YA MIJI HAPA NCHINI

(Kiwango cha juu cha joto / Kiwango cha chini cha joto)

ARUSHA 30 / 16°C

D'SALAAM 32 / 24°C

DODOMA 27 / 21°C

KIGOMA 30 / 20°C

MBEYA 23 / 16°C 

IRINGA 28 / 17°C

NJOMBE 21 / 12°C

MWANZA 26 / 19°C

TABORA 28 / 18°C

TANGA 32 / 22°C

ZANZIBAR 33 / 25°C

.....

Upepo wa Pwani: Unatarajiwa kuvuma kwa kasi ya km 30 kwa saa kwa Pwani yote; kutoka Kaskazini Mashariki kwa Pwani ya Kaskazini, na kutoka Kaskazini kwa Pwani ya Kusini.

Hali ya Bahari: Inatarajiwa kuwa na Mawimbi Makubwa kiasi.

.....

Matarajio kwa siku ya Alhamisi tarehe 21/01/2021: Kuongezeka kwa mvua katika ukanda wa Pwani ya Kusini. 

.....

Utabiri huu umetolewa leo tarehe: 19/01/2021.

Na: MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news