Utabiri wa hali ya hewa/ Weather Forecast today January 20th, 2021

 

Utabiri wa hali ya hewa wa saa 24 zijazo kuanzia saa 3 usiku wa leo Januari 19, 2021 unaletwa kwenu na mchambuzi Theresa Ngassa kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA).

Weather Forecast

Weather forecast for the next 24 hours starting 21:00 tonight on today January 19, 2021 as presented by analyst Thereza Ngassa from Tanzania Meteorological Authority (TMA).UTABIRI WA HALI YA HEWA KWA SAA 24 ZIJAZO KUANZIA SAA 3.00 USIKU WA LEO: TAREHE: 20/01/2021.

......................................................................

Mikoa ya Lindi na Mtwara inatarajiwa kuwa na Hali ya mawingu, mvua na ngurumo katika baadhi ya maeneo na vipindi vifupi vya jua.

.....

Mikoa ya Iringa, Njombe, Songwe, Mbeya, Rukwa, Morogoro na Ruvuma inatarajiwa kuwa na Hali ya mawingu, mvua na ngurumo katika maeneo machache na vipindi vifupi vya jua.

.....

Mikoa ya Kagera, Geita, Mwanza, Shinyanga, Mara, Simiyu, Kigoma, Tabora, Katavi, Dodoma na Singida inatarajiwa kuwa na Hali ya mawingu kiasi, mvua na ngurumo katika maeneo machache na vipindi vya jua.

.....

Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani (ikijumuisha Visiwa vya Mafia) inatarajiwa kuwa na Hali ya mawingu kiasi, mvua katika maeneo machache na vipindi vya jua.

.....

Mkoa wa Tanga pamoja na Visiwa vya Unguja na Pemba inatarajiwa kuwa na Hali ya mawingu kiasi, mvua nyepesi katika maeneo machache na vipindi vya jua.

.....

Mikoa ya Kilimanjaro, Manyara na Arusha inatarajiwa kuwa na Hali ya mawingu kiasi na vipindi vya jua

.....

VIWANGO VYA JOTO KWA BAADHI YA MIJI HAPA NCHINI

(Kiwango cha juu cha joto / Kiwango cha chini cha joto)

ARUSHA 29 / 17°C

D'SALAAM 32 / 24°C

DODOMA 26 / 20°C

KIGOMA 28 / 20°C

MBEYA 23 / 17°C 

IRINGA 24 / 19°C

NJOMBE 20 / 12°C

MWANZA 26 / 19°C

TABORA 28 / 18°C

TANGA 31 / 22°C

ZANZIBAR 32 / 26°C

.....

Upepo wa Pwani: Unatarajiwa kuvuma kwa kasi ya km 40 kwa saa kwa Pwani yote; kutoka Kaskazini Mashariki kwa Pwani ya Kaskazini, na kutoka Kaskazini kwa Pwani ya Kusini.

Hali ya Bahari: Inatarajiwa kuwa na Mawimbi Makubwa.

.....

Matarajio kwa siku ya Ijumaa tarehe 22/01/2021: Kuongezeka kwa mvua katika ukanda wa Pwani ya Kusini. 

.....

Utabiri huu umetolewa leo tarehe: 20/01/2021.

Na: MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA.

Post a Comment

0 Comments