HALMASHAURI ZATAKIWA KUNUNUA VIFAA VYA UPIMAJI

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Dkt. Angeline Mabula amezitaka halmashauri nchini kununua vifaa vya upimaji ardhi ili kuongeza kasi ya upimaji katika maeneo yao, anaripoti Munir Shemweta (WANMM) Bukoba.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akimkabidhi vifaa vya upimaji vyenye thamani ya milioni 34 Mkurugenzi wa Halmashauri ya Bukoba DC Solomon Kimilike wakati wa ziara yake ya kukagua utendaji kazi wa sekta ya ardhi na kuhamasishaji ulipaji kodi ya pango la ardhi katika mkoa wa Kagera tarehe 17 Februari 2021.

Aliipongeza Halmashauri ya Bukoba kwa uamuzi wake wa kutumia mapato ya ndani kununua vifaa vya upimaaji vyenye thamani ya shilingi milioni 34.

Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa vya upimaji akiwa katika ziara ya kukagua utendaji kazi wa sekta ya ardhi na kuhamasisha ukusanyaji kodi ya ardhi katika mkoa wa Kagera tarehe 17 Februari 2021, Dkt Mabula alisema ukosefu wa vifaa vya upimaji kwa halmashauri ni changamoto kubwa inayochangia kupunguza kasi ya upimaji katika maeneo mbalimbali nchini.
Sehemu ya watendaji wa sekta ya ardhi wakifuatilia maelezo yaliyokuwa yakitolewa na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula (hayupo pichani) wakati wa ziara yake ya kukagua utendaji kazi wa sekta ya ardhi na kuhamasishaji ulipaji kodi ya pango la ardhi katika mkoa wa Kagera tarehe 17 Februari 2021.

Amesema kuwa, ununuzi wa vifaa vya upimani katika halmashauri siyo tu unaongeza kasi ya upimaji ardhi katika maeneo mbalimbali bali utasaidia kuongeza wigo wa mapato kwa kuwa maeneo mengi yatakuwa yamepimwa na kuingizwa katika mfumo wa kumbukumbu za ardhi.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angeline Mabula akiangalia vifaa vya upimaji vyenye thamani ya milioni 34 alivyoikabidhi Halmashauri ya Bukoba wakati wa ziara yake ya kukagua utendaji kazi wa sekta ya ardhi na kuhamasishaji ulipaji kodi ya pango la ardhi katika mkoa wa Kagera tarehe 17 Februari 2021.

Amezishauri halmashauri zinazonunua vifaa vya upimaji kuhakikisha vifaa hivyo vinatunza na kuhifadhiwa vizuri kutokana na kuwa na thamani na umhimu mkubwa katika suala zima la upimaji.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akimkabidhi jumla ya Hati 51 za Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSF) Kaimu Meneja wa Mfuko huo mkoa wa Kagera Venant William wakati wa ziara yake ya kukagua utendaji kazi wa sekta ya ardhi na kuhamasishaji ulipaji kodi ya pango la ardhi katika mkoa wa Kagera tarehe 17 Februari 2021.

‘’Milioni 34 iliyonunua vifaa siyo fedha ndogo lazima anayehusika na kutunza vifaa awe makini na isije ikaonekana vifaa vimenunuliwa bila kutunzwa na nataka halmasahauri nyingine zione umuhimu wa kununua vifaa kwa kutumia fedha za ndani,’’amesema Dkt.Mabula.

Kwa mujibu wa Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, halmashauri zinazonunua vifaa vya upimaji zinaifanya Wizara kuangalia namna ya kuzisaidia katika zoezi zima la upangaji, upimaji na umilikishaji ardhi na kusisitiza kuwa upimaji wowote unaofanyika unafuatiwa na umilikishaji.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula (Wa pili kushoto waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na Wakurugenzi wa Halmashauri za mkoa wa Kagera wakati wa ziara yake ya kukagua utendaji kazi wa sekta ya ardhi na kuhamasishaji ulipaji kodi ya pango la ardhi katika mkoa wa Kagera tarehe 17 Februari 2021.

Aidha, katika ziara yake, Dkt Mabula aligawa Hati za ardhi kwa wamiliki wa ardhi katika halmashauri ya wilaya ya Bukoba ambapo aliwataka kuhakikisha wanalipia kodi ya pango la ardhi kwa wakati ili kuepuka kulimbikiza madeni ya kodi hiyo ambayo mwisho wa siku wataitwa wadaiwa sugu. 

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi aliwataka watendaji wa sekta ya ardhi katika halmashauri za mkoa wa Kagera kuzingatia sheria wakati wa kutekeleza majukumu yao ikiwemo kuwachukulia hatua wamiliki wanaoshindwa kulipa kodi ya pango la ardhi hata pale wanapopelekewa ilani za madai.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news