Tanzania imeandika historia mpya katika sekta ya afya baada ya wataalamu wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kufanikisha kwa mara ya kwanza upasuaji wa kupandikiza mashine za usikivu (Cochlear Implant) kwa kutumia wataalamu wa ndani pekee, bila kutegemea wataalamu kutoka nje ya nchi.
Mafanikio hayo yameelezwa kuwa hatua kubwa ya kuimarisha huduma za ubingwa bobezi nchini, kupunguza rufaa za wagonjwa kwenda nje ya nchi na kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha huduma za afya za kibingwa katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.
Akizungumza Julai 28, 2026 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili wakati wa hafla ya kuwasha mashine 13 za usikivu kwa watoto saba waliofanyiwa upasuaji mwezi Juni mwaka huu, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Bw. Emmanuel Tayari, amesema mafanikio hayo yanaakisi dhamira ya Serikali ya awamu ya sita ya kuendelea kuboresha huduma za afya na kuhakikisha wananchi wanapata matibabu ya kisasa ndani ya nchi.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo




























