Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara akutana na wadau sekta ya nguo nchini

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Exaud Kigahe amekutana na kufanya mazungumzo na wadau wa sekta nguo na mavazi ili kusikiliza changamoto wanazokutana nazo na mapendekezo yao katika kuboresha na kukuza sekta hiyo, amaripoti Mwandishi Diramakini (Dodoma)
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Exaud Kigahe akiongea na wadau wa Sekta ya Nguo na Mavazi alipokutana nao ili ksikiliza changamoto wanazokutana nazo katika uendelezaji wa Viwanda na biashara ya nguo na mavazi nchini kwenye kikao kazi cha pamoja Februari 9, 2021 jijini Dodoma.

Akizungumza na wadau hao katika kikao kilichofanyika Februari 9, 2021 katika ukumbi wa Chuo cha Biashara (CBE ) jijini Dodoma Naibu Waziri amewaagiza kuwasilisha changamoto walizonazo na rasimu za mipango mikakati ya kuboresha na kuendeleza Viwanda na Biashara katika sekta hiyo ili kukuza uchumi wa nchi.
Baadhi ya waagizaji wa nguo na mavazi hususani vitenge kutoka nje ya nchi wakimsikiliza Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Exaud Kigahe (hayupo pichani) katika kikao kilichofanyika 9 Februari 9, 2021 jijini Dodoma.

Katika kikao hicho kilichojumuisha wadau ambao ni watengenezaji na waagizaji wa nguo na mavazi kutoka nje ya nchi, wadau hao waliwasilisha changamoto na mapendekezo yao kwa Naibu Waziri wakiwa na lengo la kuboresha na kukuza sekta hiyo.
Baadhi ya waagizaji wa nguo na mavazi hususani vitenge kutoka nje ya nchi wakimsikiliza Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Exaud Kigahe (hayupo pichani) katika kikao kilichofanyika 9 Februari 9, 2021 jijini Dodoma.

Amesema Serikali imekuwa ikifanya jitihada mbalimbali katika kuendeleza sekta ya nguo na mavazi nchini ikiwemo kukuza soko la ndani la bidhaa hizo pamoja na kuandaa na kutekeleza mkakati wa kuendeleza Sekta ya pamba nguo hadi mavazi ( Cotton to Clothing Strategy C2C 2016 - 2020 ) na kuuhuisha ambapo utekelezaji wake utaanza mwaka 2021 - 2032.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news