Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mheshimiwa Dkt. Rhimo Nyansaho (Mb), tarehe 23 Julai 2026, amemwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika Mahafali ya 14 ya Chuo cha Taifa cha Ulinzi yaliyofanyika Kunduchi, jijini Dar es Salaam.
Mahafali hayo yalihitimisha mafunzo ya ngazi ya juu ya Mkakati wa Ulinzi na Usalama, ambapo jumla ya wanafunzi 72 kutoka Tanzania na nchi mbalimbali walihitimu baada ya kukamilisha mafunzo hayo.
Akizungumza kwa niaba ya Rais katika hafla hiyo, Dkt. Nyansaho alisisitiza kuwa ulinzi na usalama wa Taifa ni jukumu la kila Mtanzania, bila kujali nafasi au wajibu alionao. Alibainisha kuwa amani, utulivu na usalama wa nchi vinategemea ushirikiano wa wananchi wote katika kulinda mipaka, rasilimali na maslahi ya Taifa.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo



















