Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni amesema, kati ya jambo ambalo halipaswi kuchezewa ni Muungano ambao unatakiwa kulindwa na kila mmoja maana ndio alama kubwa ya Tanzania.


Mhe. Masauni ameyasema hayo wilayani Bagamoyo mkoani Pwani katika ziara yake ya kikazi aliyoifanya Julai 22, 2026 akieleza kufurahishwa na shughuli za maendeleo katika Mkoa wa Pwani zinazofanyika ambazo zinaunganisha na Zanzibar ikiwemo bandari.
“Fursa ya Muungano inatakiwa kusaidia pande zote bara na Zanzibar na katika hili itakuwa inasaidia zaidi kwenye sekta ya utalii kwani mtalii anapokuja Zanzibar anaunganisha na Bagamoyo kwenye hifadhi ya Saadani,” amesema.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo





























