Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Mambo ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa (SUKI), Ndugu Rabia Abdalla Hamid ameshiriki Mkutano Mkuu wa Chama cha Botswana National Front (BNF) unaofanyika mjini Jwaneng, Botswana, akiwakilisha Chama Cha Mapinduzi.
Akizungumza katika mkutano huo, Ndugu Rabia amesisitiza kuwa kila chama tawala kina wajibu wa kuwatumikia wananchi kwa uadilifu, kuimarisha misingi ya utawala bora, na kuendelea kutoa huduma zinazokidhi mahitaji ya wananchi bila kuchoka.


Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo

























