Rais Dkt.Mwinyi awaapisha majaji, Mwenyekiti Tume ya Kurekebisha Sheria Zanzibar

Majaji Wateule wa Mahakama Kuu Zanzibar wa kwanza Mhe. Ibrahim Mzee Ibrahim, Mhe. Haji Omar Haji na Mwenyekiti Mteule wa Tume ya Kurekebisha Sheria Zanzibar Bi. Khadija Shamte Mzee, wakiwa katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar wakisubiri kuapishwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Mhe.Dkt. Hussein Ali Mwinyi hafla hiyo imefanyika Februari 8,2021.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt. Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Mhe. Ibrahim Mzee Ibrahim kuwa Jaji wa Mahakama Kuu Zanzibar, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar na (kushoto kwa Rais) Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akisaini hati ya Kiapo ya Jaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar Mhe. Ibrahim Mzee Ibrahim, baada ya kumuapisha leo 8-2-2021 Ikulu Jijini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Mhe. Haji Omar Haji kuwa Jaji wa Mahakama Kuu Zanzibar, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Bi. Khadija Shamte Mzee kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Zanzibar, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Ikulu jijini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akimkabidhi Hati ya Kiapo Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Zanzibar Bi.Khadija Shamte Mzee baada ya kumaliza kula kiapo, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.
Majaji wa Mahakama Kuu Zanzibar, wakifuatilia kuapishwa kwa Majaji wa Mahakama Kuu Zanzibar na Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Zanzibar, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Ikulu jijini Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla na Jaji Mkuu wa Zanzibar, Mhe.Omar Othman Makungu wakihudhuria hafla ya kuapishwa kwa Majaji wa Mahakama Kuu Zanzibar na Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Zanzibar, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.
Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi na Utawala Bora Zanzibar, Mhe.Haroun Ali Suleiman na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi wakifuatilia kuapishwa kwa Majaji wa Mahakama Kuu Zanzibar na Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Zanzibar, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.(Picha zote na Ikulu).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news