Magazeti leo Julai 28,2026

Serikali imetangaza orodha ya wanafunzi 1,050 waliofanya vizuri zaidi katika Mtihani wa Kidato cha Sita mwaka 2026 watakaonufaika na mpango wa Samia Scholarship, ambapo wanafunzi 50 bora zaidi watapelekwa kusoma nje ya nchi katika fani za Akili Unde (Artificial Intelligence – AI), Data Science na teknolojia nyingine za kisasa.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma jana Julai 27, 2026, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda, amesema mpango huo unatekelezwa kwa maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ukiwa na lengo la kuibua na kuendeleza vipaji vya wanafunzi waliofanya vizuri katika masomo ya Sayansi, Teknolojia, Uhandisi na Hisabati (STEM) ili kuzalisha wataalamu watakaochochea maendeleo ya taifa.

Profesa Mkenda amesema kati ya wanafunzi hao, 1,000 watapata ufadhili wa kusoma katika vyuo vikuu vya ndani, huku wanafunzi 50 bora zaidi wakipewa nafasi ya kwenda kusoma nje ya nchi katika fani zinazohitajika katika uchumi wa kidijitali.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here