Tanzania yavionya vyombo vya habari nchini Kenya

Balozi wa Tanzania nchini Kenya Dkt. John Simbachawene, amevitaka vyombo vya habari vya nchini Kenya kuripoti taarifa zenye uhakika kuhusu Tanzania na kuacha kutoa maneno yenye kuleta hofu kwa watu, anaripoti Mwandishi Maalum (EATV).

Balozi Simbachawene ametoa kauli hiyo hii leo wakati akizungumza na EATV, ofisini kwake Jijini Nairobi nchini Kenya, baada ya chombo kimoja cha habari nchini Kenya kuripoti taarifa za uwepo wa taharuki za ugonjwa wa Corona nchini Tanzania jambo ambalo si la kweli.

Mbali na hayo Balozi Simbachawene, amewataka Watanzania kuendelea kuchukua tahadhari za COVID-19, na kueleza kuwa Tanzania imekuwa mstari wa mbele kuhakikisha wananchi wanafuata ushauri wa wataalamu na Wizara ya Afya pamoja na miongozo inayotolewa na Shirika la Afya Duniani (WHO).

Aidha, ametoa rai kwa Watanzania wanaotaka kwenda nchini Kenya kuhakikisha wana nyaraka hitajika kwa mujibu wa Wizara ya Afya, na wale wanaoishi nchini humo amewasihi kufuata kanuni na masharti yaliyowekwa kupambana na ugonjwa wa COVID-19.
Balozi wa Tanzania nchini Kenya Dkt. John Simbachawene

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news