Waziri Mabula aagiza viwanja vilivyoidhinishwa ramani za upimaji kutozwa kodi

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angeline Mabula amezitaka idara za ardhi katika halmashauri za mkoa wa Shinyanga kuwatambua wamiliki wote wa ardhi ambao ramani za upimaji wa viwanja vyao umeidhinishwa na kuanza kuwatoza kodi ya pango la ardhi kwa mujibu wa sheria, anaripoti Munir Shemweta-WANMM) Shinyanga.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo Makazi Dkt Angeline Mabula akizungumza na Watendaji wa Sekta ya Ardhi katika mkoa wa Shinyanga wakati wa ziara ya siku moja ya kikazi katika mkoa huo tarehe leo Februari 1, 2021. (Picha na Munir Shemweta-WANMM).

Dkt.Mabula ametoa agizo hilo leo Februari 1, 2021 mkoani Shinyanga wakati wa ziara yake ya siku moja kukagua utendaji kazi wa sekta ya ardhi, kuhamasisha ukusanyaji kodi ya pango la ardhi pamoja na kukutana na makampuni ya urasimishani.

"Kila halmashauri katika mkoa huu wa Shinyanga ichukue hatua kwa kuwatambua wamiliki wote wa viwanja ambao approved survey imefanyika na kuanza kuwatoza kodi ya pango la ardhi,"amesema Dkt.Mabula.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo Makazi, Dkt Angeline Mabula akimkabidhi Hati mmoja wa wakazi wa Manispaa ya Shinyanga wakati wa zoezi la kutoa hati akiwa katika ziara ya kikazi katika mkoa wa Shinyanga. Kulia ni Kamishna wa Ardhi Msaidizi mkoa wa Shinyanga, Ezekiel Kitlya. (Picha na Munir Shemweta-WANMM).

Kwa mujibu wa Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt.Mabula kwa sasa hakuna suala la kubembeleza wakati wa kufuatilia wadaiwa wa kodi ya ardhi na kusisitiza kuwa shilingi bilioni 1.3 sawa na asilimia 22 zilizokusanywa kufikia Desemba 2020 kama kodi ya ardhi katika mkoa wa Shinyanga ni ndogo na aibu kwa mkoa.

Kwa mujibu wa Kamishna wa Ardhi Msaidizi wa Ardhi mkoa wa Shinyanga, Ezekiel Kitlya, mkoa huo hadi kufikia Desemba 2020 imekusanya kiasi cha shilingi bilioni 1.3 kama kodi ya pango la ardhi katika halmashauri za mkoa wa Shinyanga.

Aidha, amewataka maafisa ardhi katika halmashauri za mkoa wa Shinyanga kuwafutia viwanja wamiliki wa adhi waliokaidi kulipa kodi ya pango la ardhi hata pale walipopelekewa ilani za madai baada ya miezi sita.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo Makazi, Dkt Angeline Mabula akiwa katika picha ya pamoja na wananchi wa Manispaa ya Shinyanga aliowakabidhi hati za ardhi akiwa katika ziara ya kikazi katika mkoa wa Shinyanga leo Februari 1, 2021. Kulia ni Kaimu Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga, Beda Chamatata na wa pili kulia ni Kamishna wa Ardhi Msaidizi mkoa wa Shinyanga Ezekiel Kitlya. (Picha na Munir Shemweta-WANMM).

Kwa mujibu wa kifungu Na 48(1) (g) cha sheria ya ardhi, Afisa Ardhi anayo mamlaka ya kufuta umiliki wa ardhi kwa mmiliki aliyekaidi kulipa kodi ya pango la ardhi katika kipindi cha miezi sita baada ya kutumiwa ilani ya madai.

"Hatua zisipochukuliwa katika suala lla kudai kodi ya ardhi kwa wadaiwa sugu hatutaitendea haki Tanzania katika mapato ambayo yanamsaidia Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli kutekeleza miradi ya maendeleo,"amesema Naibu Waziri Mabula.

Aidha, Naibu Waziri Mabula katika ziara yake alitoa hati kumi na moja kati ya kumi na tisa kwa wananchi wa Manispaa ya Shinyanga na kuwataka waliokabidhiwa hati kuhakikisha wanalipa madeni yao katika kipindi cha siku kumi nne na wasipofanya hivyo wafikishwe kwenye Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya kwa hatua zaidi.

Kwa mujibu wa Naibu Waziri Dkt.Mabula faida ya hati ni pamoja na kuwa na usalama wa miliki, kuepuka migogoro ya ardhi inayoweza kusababishwa na mipaka pamoja na kuitumia hati katika shughuli za maendeleo kwa kuchukulia mkopo benki.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news