Habari katika picha kuhusu Mkutano wa Tume ya Utumishi wa Umma jijini Dar es Salaam leo Machi 15, 2021

Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Umma Mheshimiwa jaji (mstaafu), Dkt.Steven J. Bwana (katikati) akizungumza wakati wa Mkutano wa Tume ulioanza leo jijini Dar es Salaam, ambapo rufaa na malalamiko ya watumishi yaliyowasilishwa Tume yatatolewa uamuzi. Wengine ni Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Umma Mheshimiwa George D. Yambesi (kushoto) na Bw. John Mbisso, Kaimu Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma (kulia). (Picha na PSC).
Kamishina wa Tume ya Utumishi wa Umma, mheshimiwa Balozi (mstaafu) Daniel Ole Njoolay (kulia) akisisitiza jambo wakati wa Mkutano wa Tume unaofanyika jijini Dar es Salaam kujadili na kutoa uamuzi wa rufaa na malalamiko ya watumishi wa umma yaliyowasilishwa Tume, kushoto kwake ni Kamishna wa Tume mheshimiwa Balozi (mstaafu) John Haule (picha na PSC).
Kaimu Katibu wa Tume Bw. John Mbisso (katikati) akiwasilisha taarifa wakati wa Mkutano wa Tume ulioanza leo jijini Dar es Salaam, wengine ni Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Umma, mheshimiwa Jaji (mstaafu) Dk. Steven Bwana (kushoto) na Kamishna wa Tume mheshimiwa Balozi (mstaafu) John Haule. (Picha na PSC).
Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Umma mheshimiwa Jaji (mstaafu) Dk. Steven Bwana (kushoto) akizungumza leo jijini dar es Salaam wakati wa Mkutano wa tume, wengine ni Bw. John Mbisso (Kaimu Katibu wa Tume), Kamishna wa Tume, mheshimiwa Balozi (mstaafu) John Haule na Mheshimiwa Balozi (mstaafu) Daniel Ole Njoolay, Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Umma. (Picha na PSC).

Post a Comment

0 Comments