TUME ya Ushindani (FCC) kupitia Kanda ya Ziwa imeendelea kusogeza huduma karibu na wananchi kwa kutoa elimu ya ulinzi wa mlaji kupitia Kliniki ya Mlaji inayofanyika katika viwanja vya Shule ya Msingi Mkendo, Manispaa ya Musoma.
Katika kuimarisha uelewa wa wadau mbalimbali, FCC haikuishia kwa wananchi pekee bali pia ilifanya ziara maalum kwa baadhi ya taasisi zinazotoa huduma ndogo za fedha katika manispaa hiyo, kwa lengo la kuzielimisha juu ya wajibu wao wa kuzingatia sheria na kanuni katika utoaji wa huduma.
Akiongoza zoezi hilo, Mkuu wa Kanda ya Ziwa,Bw. Frank Mdimi, akishirikiana na Afisa Biashara wa Manispaa ya Musoma, Joshua Mlole pamoja na maafisa wengine, walitembelea taasisi za Enokwe, Pongeza na Ohura na kufanya mazungumzo ya moja kwa moja na watoa huduma hao.
Katika ziara hiyo, maafisa wa FCC wamesisitiza umuhimu wa kuandaa mikataba ya huduma kwa uwazi na haki, wakielekeza taasisi hizo kuzingatia matakwa ya Sheria ya Ushindani inasimamia na kudhibiti Mikataba ya Mlaji inayoandaliwa na watoa huduma.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo
























