Magazeti leo Machi 31,2026

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo, imetoa vifaa vya TEHAMA vyenye thamani ya jumla ya Sh. 769,390,000 kwa shule za msingi na sekondari 19 zilizopo katika mikoa tisa ya Tanzania Bara na Zanzibar.
Vifaa hivyo vinajumuisha madarasa janja, mbao janja, vishikwambi na kompyuta, ambavyo vinatarajiwa kuwezesha ujifunzaji kwa wanafunzi, hususan katika masomo ya sayansi na teknolojia. Aidha, walimu watanufaika kwa kutumia mbinu bunifu za ufundishaji pamoja na mifumo ya kidijitali kufuatilia maendeleo ya wanafunzi kwa ufanisi zaidi.

Hafla ya ugawaji wa vifaa hivyo imefanyika Machi 30, 2026 jijini Dodoma, ambapo Naibu Waziri wa Elimu, Mhe. Wanu Hafidh Ameir, alisisitiza dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita kuendeleza mageuzi makubwa katika sekta ya elimu kupitia matumizi ya teknolojia za kidijitali.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here