Serikali yawaasa Wafungwa kufanya ibada

Serikali imewaasa wafungwa wote nchini kuzidisha kufanya ibada sambamba na kuzidisha kumuomba mungu ili wakitoka waende kuwa raia wema Pamoja na kukamilisha ndoto zao walizokua nazo, anaripoti Mwandishi DIRAMAKINI.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Khamis Hamza Chilo katika kikao kikao cha ndani kilichohusisha wafungwa na mahabusu katika gereza la wilaya ya Sindida mjini ambapo pia alipata fursa ya kuwasikiliza wafungwa ambao walitoa maoni,mapendekezo na changamoto mbalimbali walizokua nazo ikiwemo kuchelewa kwa upepelezi wa kesi zao.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Khamis Hamza Chilo(wapili kulia), akiwaongoza Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama vilivyopo chini ya wizara hiyo, kula chakula kinacholiwa na wafungwa pia katika Gereza la Wilaya ya Singida,ambapo baada ya chakula hicho alipata fursa ya kuzungumza na wafungwa hao. (Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi).

“Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anawategemea sana hasa vijana na Taifa hili linawategemea sana,hapa naona vijana mko wengi vijana ndio nguvu kazi ya Taifa,sasa endeleeni kuwa raia wema,ukitoka hapa kifungoni nenda kawe raia mwema,mkitoka hapa nendeni mkaendeleze ndoto zenu,fanyeni ibada muombeni mungu sana fanyeni ibada huwezi kujua ukitoka hapa utaenda kuwa nani maana historia inatuonyesha wako watu mbalimbali walikua wafungwa lakini walivyomaliza vifungo vyao walienda kuwa viongozi wakubwa tu,"amesema Naibu Waziri Chilo.

Akisoma taarifa ya gereza mbele ya Naibu Waziri, Mkuu wa Gereza la Wilaya ya Singida, amesema katika gereza hilo kuna shughuli mbalimbali za uzalishaji ikiwemo kilimo cha mahindi, maharage, kilimo cha mbogamboga,ufyatuaji wa tofali,ufugaji wa Samaki,ujenzi wa nyumba za makazi ya askari.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news