Waziri Biteko atoa wito kwa Taasisi ya TEIT

Waziri wa Madini, Doto Biteko ameitaka Taasisi ya Uhamasishaji Uwazi na Uwajibikaji katika Rasilimali za Madini, Mafuta na Gesi asilia (TEIT) kufanya kazi kwa bidiii ikiwa ni pamoja na kuonesha uwepo wa kazi zake ambazo imekuwa ikizifanya, anaripoti Mwandishi DIRAMAKINI (Dar es Salaam).
Waziri wa Madini Doto Biteko (katikati), kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Taasisi ya Uwazi na Uwajibikaji katika Rasilimali Madini, Mafuta na Gesi Asilia (TEITI) na kulia ni Kaimu Katibu Mtendaji wa Mariam Mgaya wakiwa kwenye Kikao kilichofanyika Machi 10, 2021 katika Ukumbi wa Samwel Sita uliopo katika Ofisi za Bunge jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Madini Doto Biteko kulia akizungumza na Mwenyekiti wa Kamati ya Taasisi ya Uwazi na Uwajibikaji katika Rasilimali Madini, Mafuta na Gesi Asilia (TEITI) Ludovick Utouh kwenye kikao cha Waziri wa Madini Doto Biteko, kilichofanyika Machi 10, 2021 katika Ukumbi wa Samwel Sita uliopo katika Ofisi za Bunge jijini Dar es Salaam.
Mheshimiwa Waziri Biteko ametoa agizo hilo leo Machi 10, 2021 jijini Dar es Salaam wakati alipokuwa akizungumza na watendaji wa Taasisi ya TEIT katika Ukumbi wa Samwel Sitta uliopo katika ofisi ndogo za Bunge jijini humo

Biteko amesema, elimu ni moja ya jukumu muhimu ambalo TEIT inapaswa kuitumia katika kazi zake ili kuweza kuwafikia wananchi kwa urahisi zaidi kwa kutumia njia ya kujitangaza ili waweze kuelewa zaidi sekta ya madini,mafuta na gesi asilia.

"TEIT ni miongoni mwa taasisi namba moja ambayo inapaswa kufanya kazi zake kwa kujisimamia na kujiendesha yenyewe badala ya kusubiri kuwezeshwa na badala yake itumie rasiliamali zake kujiendeleza yenyewe," amesema Waziri Biteko.
Mwenyekiti wa Kamati ya Taasisi ya Uwazi na Uwajibikaji katika Rasilimali Madini, Mafuta na Gesi Asilia (TEITI) Ludovick Utouh akizungimza jambo kwenye kikao cha Waziri wa Madini Doto Biteko, kilichofanyika Machi 10, 2021 katika Ukumbi wa Samwel Sita uliopo katika Ofisi za Bunge jijini Dar es Salaam.

Biteko ametaka taasisi hiyo kutumia ripoti zake ambazo imekuwa ikizalisha kujitangaza zaidi kwani kufanya hivyo kutaiwezesha TEIT kufika mbali zaidi na kutambulika katika jamii.

Amesema, katika ufanyaji kazi wa taasisi hiyo inapaswa kuacha kulalamika na kulaumu na badala yake ijikite katika kufanya kazi ili iweze kuhakikisha sekta ya madini, mafuta, gesi zinasonga mbele.

"Nyinyi ndio mnaweza kuiwezesha TEIT kujulikana, hivyo fanyeni kazi kwa kuonesha kazi zenu ambazo zitawawezesha kuonekana na kutambulika katika jamii na hatimaye kufika mbali zaidi,"amesema Biteko.

Kwa upande wake Kaimu Katibu Mtendaji TEIT, Mariam Mgaya alisema TEIT imejipanga kukamilisha na kuweka wazi kwa umma ripoti ya ulinganishi wa malipo ya kampuni za madini,mafuta, gesi asilia sambamba na mapato ya serikali kwa mwaka wa fedha 2018/19 na 2019/20.
Kaimu Katibu Mtendaji wa Taasisi ya Uwazi na Uwajibikaji katika Rasilimali Madini, Mafuta na Gesi Asilia (TEITI) akiwasilisha mada katika Kikao cha Waziri wa Madini Doto Biteko na Wajumbe wa TEITI kilichofanyika Machi 10, 2021 katika Ukumbi wa Samwel Sita uliopo katika Ofisi za Bunge jijini Dar es Salaam.

Amesema, katika matarajio hayo pia itaanzisha mfumo wa kielektroniki utakaotumia na kampuni pamoja na taasisi za Serikali kuripoti yaliofanywa na kampuni hizo kwa serikali.

Aidha, amesema TEIT imekuwa ikikabiliwa na chagamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na upungufu wa watumishi kulingana na majukumu yake.
Kaimu Katibu Mtendaji wa Taasisi ya Uwazi na Uwajibikaji katika Rasilimali Madini, Mafuta na Gesi Asilia (TEITI) akiwasilisha mada katika Kikao cha Waziri wa Madini Doto Biteko na Wajumbe wa TEITI kilichofanyika Machi 10, 2021 katika Ukumbi wa Samwel Sita uliopo katika Ofisi za Bunge jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Wajumbe wa Taasisi ya Uwazi na Uwajibikaji katika Rasilimali Madini, Mafuta na Gesi Asilia (TEITI) waliohudhulia Kikao cha Waziri wa Madini Doto Biteko, kilichofanyika Machi 10, 2021 katika Ukumbi wa Samwel Sita uliopo katika Ofisi za Bunge jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Madini Doto Biteko akizungumza jambo kwenye kikao kati yake na Wajumbe wa Taasisi ya Uwazi na Uwajibikaji katika Rasilimali Madini, Mafuta na Gesi Asilia (TEITI) kilichofanyika Machi 10, 2021 katika Ukumbi wa Samwel Sita uliopo katika Ofisi za Bunge jijini Dar es Salaam.

"Kwa sasa TEIT inashirikiana na wizara kufuatilia muundo wa TEIT katika mamlaka husika ili kuweza kutatua chagamoto ya upungufu wa watumishi,"amesema Mgaya.

Pia amesema, TEIT itaendelea kuhakikisha serikali inaweka mifumo ya uwazi katika usimamizi wa rasiliamali madini,mafuta na gesi asilia ili kuboresha ukusanyaji wa mapato na manufaa yanayotokana na shughuli za utafutaji na uchimbaji rasiliamali hizo nchini.

Post a Comment

0 Comments