KMC FC KUWAKABILI RUVU SHOOTING KESHO KATIKA UWANJA WA UHURU

Kikosi cha KMC FC kipo tayari katika mpambano wa kesho dhidi ya Ruvu Shooting na kwamba maandalizi yamekamilika kwa asilimia kubwa hivyo mashabiki na wapenzi wajitokeze kwa wingi ili kushuhudia mtanange huo wenye mvuto kutoka kwa wana Kino Boys.
KMC FC kesho itakuwa katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam kwenye mchezo wa Ligi kuu Soka Tanzania bara dhidi ya Ruvu mchezo utakaopigwa saa 16.00 jioni na kwamba hali za wachezaji ziko vizuri na hakuna majeruhi katika kikosi hicho.

Kino Boys kupitia kwa makocha wake wazawa, John Simkoko Kocha Mkuu na Habibu Kondo, Kocha msaidizi wapo kwenye hali nzuri na kwamba maandalizi yaliyofanywa na makocha hao nikuhakikisha kwamba Timu inapata matokeo mazuri katika uwanja wake wa nyumbani.

KMC FC imetoka kupoteza mchezo mmoja ugenini dhidi ya Polisi Tanzania na kupata sare dhidi ya Coast katika uwanja wa Mkwawani Jijini Tanga na kwamba katika mchezo wa kesho wachezaji wote wanamorali ya kuhakikisha kwamba wanapa alama tatu na hivyo kupanda katika nafasi ya juu kwenye msimamo Ligi Kuu soka Tanzania bara.

Maandalizi tulishafanya muda mrefu, tunachosubiria ni dakika tisini za mchezo wa kesho tunamalizaje, kama Timu tunakwenda kupambana kuhakikisha alama tatu zinapatikana kwasababu tunacheza nyumbani, licha ya kwamba tunakutana na Timu ngumu lakini pia tupo kwenye mzunguko wa mwisho hivi sasa hivyo tunahitaji kushinda.

KMC FC hadi sasa ipo katika nafasi ya saba kwenye msimamo ya Ligi kuu Soka Tanzania Bara ikiwa imeshacheza michezo 23 na kujikusanyia alama 32 na kwamba inahitaji ushindi katika mchezo wa kesho ili kutoa burudani zaidi kwa mashabiki zake.

Imetolewa na Christina Mwagala

Afisa Habari na Mawasiliano wa Timu ya KMC FC

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news