COSOTA KUSIMAMIA HAKIMILIKI YA SANAA ZA UFUNDI KATIKA MFUMO WA MAUZO KWA MTANDAO

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Innocent Bashungwa ameagiza COSOTA na BASATA kuandaa mfumo wa kuuza kazi za Wachoraji na Wachongaji kwa njia ya mtandao,anaripoti  Anitha Jonas  (COSOTA) Dar es Salaam.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa akitoa maelekezo kwa COSOTA na BASATA kuandaa mfumo wa kuuza kazi za Wachoraji na Wachongaji kwa njia ya mtandao kufuatia ukuaji wa teknolojia na uwanda mpana wa masoko katika mfumo wa mtandao au programu za simu ’Apps’ leo Machi 15,2021 Jijini Dar es Salaam katika kikao wadau wa Sanaa ya Uchoraji na Uchongaji kilicholenga kutatua changamoto zinazowakabili.

Mheshimiwa Bashungwa ametoa agizo hilo leo Jijini Dar es Salaam katika kikao chake na Wasanii wa Sanaa ya Uchoraji na uchongaji nchini kilicholenga kutatua changamoto Zinazowakabili katika uendeshaji wa kazi zao ikiwemo suala la masoko.

“Katika karne hii ya 21 suala la Masoko linafanyika kwa njia ya mtandao na njia hii ni rahisi na inatangaza biashara kwa haraka zaidi na katika hili COSOTA mtatakiwa kuhakikisha mnalinda Hakimiliki za kazi hizo,”alisema Mhe.Bashungwa.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Hakimiliki na Hakishiriki Tanzania Doreen Sinare akiwasisitiza wanachama wa Tingatinga Arts kusajili kazi zao badala ya kusubiri mpaka wanapopata changamoto ndiyo wanakumbuka kujisajili, katika kikao na wadau wa Sanaa ya Uchoraji na Uchongaji kilichofanyika leo Jijini Dar es Salaam leo Machi 15,2021 kwa lengo la kutatua changamoto zinazowakabili.

Akiendelea kuzungumza katika mkutano huo Waziri huyo aliwasihi Wachoraji na Wachongaji kusajili kazi zao COSOTA ili ziweze kulindwa, pia alitoa msisitizo kwa wadau hao kuhakikisha wanawasiliana BASATA pamoja na COSOTA pale wanapokuwa na mikataba yao kibiashara kwa lengo la kupata ushauri wa kisheria ili kuweza kulinda kazi hiyo pamoja na maslahi yake.

Pamoja na hayo naye Afisa Mtendaji Mkuu na Msimamizi wa Hakimiliki Tanzania (COSOTA) Bibi.Doreen Sinare alieleza kuwa taasisi hiyo imetengeneza Kanuni mpya ambazo zitawasaidia Wachoraji na Wachongaji kunufaika na kazi zao baada ya kuuza kazi zao na kazi hizo kwenda kuuzwa tena nje ya nchi kupitia minada na njia nyingine kama hizo ambapo kazi huuzwa kwa bei za juu ilihali msanii kutokupata chochote kutokana na mauzo hayo zijulikanazo kama ‘resale royalties rights’.

“Napenda kuwasisitiza kuhusu suala la kusajili kazi zenu kuna wakati nilitembelea ofisi za Tingatinga na nikawashauri kuhusu suala la kusajili kazi zenu COSOTA lakini baadhi yenu walikuja ila wengine hawakuja sasa naendelea kuwasisitiza kusajili msisubiri mpaka mnapopata changamoto ndiyo mnaanza kuhangaika,”alisema Bibi.Doreen.
Rais wa Shirikisho la Sanaa za Ufundi Bw.Andrian Nyangamale akitoa ombi kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa kwa niaba ya Wasanii wa Sanaa ya Ufundi kuwa wanaomba Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anapokuwa akitoa zawadi ya Sanaa hizo kwa wageni kutaja jina la Mchoraji au Mchongaji wa kazi hiyo kwa lengo la kusaidia kumtangazia biashara , leo Machi 15,2021 Jijini Dar es Salaam katika kikao na wadau wa Sanaa ya Uchoraji na Uchongaji kilicholenga kutatua changamoto zinazowakabili.

Pamoja na hayo Mtendaji huyo alieleza dhamira yake ya kutembelea eneo la biashara ya vinyago Mwenge Machi 19, 2021 kwa lengo la kuwapa elimu ya Hakimiliki na Hakishiriki ili kuwaongezea uelewa wa masuala hayo ikiwemo maboresho ya Kanuni mbalimbali zinazosimamia hakimiliki.

Pamoja na Kituo cha Wachoraji wa Sanaa ya Tingatinga Oysterbay ambapo itakuwa ni mara nyingine anawatembelea  
Katibu wa Tingatinga Arts Tanzania Bw. … akiwasilisha akimwomba Mheshimiwa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa kumsaidia kutatua changamoto ya mgogoro wa mipaka ya Kiwanja cha Ofisi yao Oysterbay leo Machi 15,2021 jijini Dar es Salaam katika kikao wadau wa Sanaa ya Uchoraji na Uchongaji kwa kilicholenga kutatua changamoto zinazowakabili.

Mbali na hayo Bibi.Doreen alitangaza napenda kutoa ofa kwa wanawake wanaofanya kazi ya Sanaa ya Ufundi kupamba Ofisi ya COSOTA kwa kazi zao ikiwemo kwa Sanaa ya uchoraji au uchongaji

Kufuatia mgogoro wa Tingatinga Arts na Kampuni ya Kenya Mtendaji Mkuu wa COSOTA aliwaelekeza viongozi wa chama hicho kumpeleka mkataba wao katika Ofisi yake ili aweze kutoa ushauri.  
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa (aliyeketi wanne kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wasanii wa Sanaa ya uchoraji na uchongaji mara baada ya kikao na wadau hao kilichofanyika leo Jijijini Dar es Salaam kilicholenga kujadili changamoto zinazowakabili, aliyeketi ni watatu kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu na Msimamizi wa Hakimiliki Tanzania (COSOTA) Doreen Sinare.

Pamoja na hayo Katika kikao Waziri Bahungwa alisisitiza mikataba huo ufuatiliwe na COSOTA, na kama kuna haki za Tingatinga basi haki hizo zifuafuatiliwe na zipatikane hii ni kutokana na sintofahamu ya kusemekana kuwepo kwa baadhi ya wasanii ambao walisaini na kulipwa kwa kazi hiyo. Hivyo mkataba ndio utatoa picha kamili.

Kwa upande Rais wa Shirikisho la Sanaa za Ufundi Bw.Andrian Nyangamale alitoa ombi kwa Serikali kuwa anaomba katika zawadi zile za vinyago au picha za kuchorwa zinazotolewa kwa wageni Ikulu basi Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ataje jina la aliyefanya fanya kazi hiyo pale anapokabishi. *Mh. Waziri alipokea na kuahidi kufanyia kazi jambo hilo.

Post a Comment

0 Comments