BRELA yakaribisha wajasiriamali kurasimisha biashara zao

Wadau wa bishara na wamiliki wa viwanda vidogovidogo katika Mkoa wa Njombe wametakiwa kutumia elimu inayotolewa na Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) na kuwaelimisha wengine ili waweze kurasimisha biashara zao ili ziweze kutambulika kisheria, anaripoti Christina Njovu (BRELA) Njombe.

Akizungumza wakati wa warsha ya utoaji elimu ana kwa ana juu ya huduma zinazotolewa na BRELA iliyofanyika katika ukumbi wa SIDO mkoani Njombe Mwenyekiti wa TCCIA Mkoa wa Njombe Menerad Mlyuka amesema kuwa;
Afisa Leseni Rajab Chambega akitoa elimu juu ya namna ya upataji wa leseni za viwanda na biashara katika semina kwa wajasiliamali na wafanya biashara iliyofanyika katika ukumbi wa SIDO mkoani Njombe.

“Elimu hii inayotolewa na BRELA ni muhimu kila mmoja akasikiliza kwa makini na kuielewa ,Kila mmoja asikilize na apate ufahamu ili akaweze kuitumia hii elimu vizuri zaidi na akawafundishe na wengine , kwa kutumia pia vyombo vya habari vilivyoshiriki natumaini elimu hii itaweza kuenea katika mkoa mzima wa Njombe” alisema Mlyuka.

Wakitoa pongezi kwa BRELA kwa kuamua kutoka na kuwapatia elimu hiyo mmoja wa washiriki hao bibi Roida Emanuel Mng’ong’o ambaye ni mjasiliamali wa usindikaji wa asali na pia ni muuzaji wa asali alieleza kuwa aliwahi kupata elimu kuhusu BRELA kutoka kwa watu ambao sio sahihi kiasi ambacho alishindwa kuelewa nini afanye katika kuendelea kuhuisha biashara yake.
Wafanyakazi wa BRELA wakitia elimu kwa umma juu ya huduma zinazitolewa na Wakala katika kituo cha redio Uplands kilichopo Mkoani Njombe.

Kutokana na elimu hii iliyotolewa na BRELA Mkoani Njombe imemuwezesha kuifahamu vizuri BRELA ikiwa ni pamoja na kutambua kuwa anatakiwa kuhuisha biashata yake kila mwaka ili iweze kutambulika ndani ya nchi hata nje ya nchi.

Aidha washiriki hao walitoa mapendekezo yao ya kutaka taasisi nyingine zinazotoa huduma kama BRELA kushirikiana kwapamoja katika kutoa elimu ili wadau waweze kutambua mipaka na majukumu ya kila taasisi ambazo walizitaja baadhi kuwa ni pamoja na TBS na TRA na TFDA.
baadhi ya washriki wakifuatilia Semina ya utoaji elimu juu ya namna ya upataji wa huduma zitolewazo na BRELA zikiwemo upataji Leseni za viwanda na biashara katika semina kwa wajasiliamali na wafanya biashara iliyofanyika katika ukumbi wa SIDO mkoani Njombe.

Wameongeza kuwa BRELA inatakiwa kutoka ofisini na kufika hadi katika wilaya ili wafanyabishara na wadau wa biashara waweze kupata huduma stahiki kwa usahihi kutoka kwa wahusika wakuu tofauti na ilivyo sasa ambapo baadhi ya wale wanaojiita BRELA wanashindwa kuwahudumia ipasavyo badala ya mteja kuondoka akiwa ameridhika badala yake anaondoka akiwa na sononeko.

BRELA ipo katika kazi ya kutoa elimu kwa umma mkoani njombe ambapo pamoja na kukutana na wadau ana kwa ana pia imetoa elimu hiyo kwa njia ya redio za kijamii ili wananchi hadi walio vijijini waweze kuelewa namna ya urasimishaji biashara zao kwa kusajili majina na alama za biashara zao na kuacha kutumia vyeti vya watu wengine katika kutoa huduma ama kufanya biashara.

Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni inafanya kazi zake kwa njia ya mtandao, ambapo mtu yeyote anayehitaji kufanya sajili atapata hiyo huduma kwa njia ya mtandao, ikiwa atakumbana na changamoto atatakiwa kupiga namba +255 (0)222 212 800 ambapo ataweza kupata maelekezo zaidi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news