MHANDISI MASAUNI AWATAKA VIJANA KUCHANGAMKIA FURSA ZA UCHUMI WA BLUU ZANZIBAR

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni amewahimiza vijana Visiwani Zanzibar kuchangamkia fursa za uchumi wa blue unaotokana na shughuli za uvuvi na uchakataji wa samaki ili waweze kujikwamua kiuchumi, anaripoti Benny Mwaipaja WFM) Zanzibar.

Mhe. Masauni ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni-Zanzibar, ametoa rai hiyo wakati akizungumza na viongozi na baadhi ya wanachama wa Chama cha Mapinduzi katika Jimbo la Kikwajuni akiwa katika ziara yake ya kikazi visiwani humo.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni (Mbunge wa Kikwajuni, katikati), akizungumza na wananchi wa Jimbo la Kikwajuni, Zanzibar, kuhusu utekelezaji wa miradi ya maendeleo hususani uchumi wa Blue, kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) katika Jimbo hilo, Bi. Mvita Mussa Kibendera na kulia ni Katibu Mwenezi wa Jimbo hilo, Bw. Ismail Malik Mohd.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni (Mbunge wa Kikwajuni), (kushoto), akizungumza na wananchi wa Jimbo la Kikwajuni, alipofanya ziara ya kikazi jimboni humo kutatua changamoto mbalimbali zikiwemo za miradi ya maendeleo.

Amesema kuwa yeye binafsi na Mwakilishi wa Jimbo hilo katika Baraza la Wawakilishi Mhe. Nasor Ali Jazeerah pamoja na viongozi wengine wamejipanga kutoa vifaa vitakavyotumiwa na vijana kwa ajuili ya shughuli za uvuvi katika sekta hiyo ya uchumi wa blue ili waweze kujitegemea kwa kujipatia kipato cha uhakika.

“Tunataka tuangalie uwezekano wa kujenga mazingira mazuri ya kuwatafutia “ndoano” na siyo “samaki” na tumeandaa vitu vikubwa ambavyo sitaki niseme mapema hapa nitaondoa radha, mkawaambie vijana wa Kikwajuni kama hawatatoka kimaisha kipindi hiki hawatatoka maisha” alilisisitiza Mhe. Masauni.
Baadhi ya Wazee wa Kikwajuni Zanzibar, wakifuatilia maelezo ya Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni (Mbunge wa Kikwajuni) (hayupo pichani), kuhusu mipango ya maendeleo ya Jimbo la Kikwajuni.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Jimbo la Kikwajuni, Bi. Mvita Mussa Kibendera, akiwataka wananchi kushirikiana na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni (Mb) wa Jimbo hilo (hayupo pichani), katika kuliletea maendeleo jimbo hilo. Wananchi wa Jimbo la Kikwajuni, Zanzibar wakifuatilia maelezo ya Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni, (Mbunge wa Kikwajuni, (hayupo pichani), alipotembelea jimbo hilo kwa lengo la kutatua changamoto mbalimbali za wananchi, katika juhudi za kuwaletea maendeleo.
Mzee Rajabu Mohamed mkaazi wa Kikwajuni, akieleza kufurahishwa na juhudi za Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni (Mbunge wa Kikwajuni), katika kuwaletea maendeleo wananchi wake.(Picha na Peter Haule, WFM, Zanzibar).

Pamoja na kusisitiza masuala ya kiuchumi, Mhandisi Masauni alisema kuwa mipango mingine iliyowekwa na uongozi katika Jimbo la Kikwajuni ni kuendesha mashindano ya kusoma qoran kwa vijana na kuwataka wazazi kuwahimiza watoto wao kushiriki mashindano hayo.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Jimbo hilo Mhe. Nasor Ali Jazeerah, aliwaahidi wakazi wa Jimbo la Kikwajuni-Zanzibar kwamba ahadi zote zilizoahidiwa wakati wa Uchaguzi Mkuu uliopita zitatekelezwa kikamilifu.

Alitoa wito kwa wakazi wa Jimbo hilo kushikamana, kupendana na kuacha majungu ili mipango ya maendeleo iliyopangwa iweze kutekelezwa kwa kasi zaidi.

Aliwashukuru wananchi kwa kumwombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ili waendelee kuingoza nchi kwa umahili mkubwa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news