TAKUKURU yamnasa kigogo wa Bandari aliyekuwa mafichoni

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU)Mkoa wa Mwanza, imemnasa akiwa mafichoni aliyekuwa Mhasibu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA),Kigoma, Madaraka Robert Madaraka, anaripoti Mwandishi DIRAMAKINI (Mwanza).

Madaraka anatuhumiwa kwa makosa ya rushwa,uhujumu uchumi na ukwepaji kodi wa sh.153,543,550,alinaswa na taasisi hiyo Aprili 19,mwaka huu akiwa amejificha eneo la Nyasaka,Manispaa ya Ilemela.

Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Mwanza, Frank Mkilanya akizungumza na waandishi wa habari wakati akitoa taarifa ya utendaji wa taasisi hiyo katika kipindi cha Januari hadi Machi,mwaka huu amesema mtuhumiwa huyo alikuwa akitafutwa tangu Agosti 2020.

Amesema, Madaraka alikuwa akitafutwa na TAKUKURU ili aunganishwe na watuhumiwa wenzake watano,waliokuwa watumishi wa TPA mkoani Kigoma,ambapo alikamatwa akiwa amejificha huko Nyasaka, katika Manispaa ya Ilemela jijini Mwanza.

“TAKUKURU Mkoa wa Mwanza,mnamo Aprili 19,2021,ilimkamata aliyekuwa Mhasibu wa Mamlaka ya Bandari Kigoma,Madaraka Robert Madaraka ambaye alikuwa akituhumiwa kwa makosa ya rushwa,uhujumu uchumi na ukwepaji kodi wa kiasi cha sh. 153,543,550,”amesema Mkilanya.

Amewataja watuhumiwa wengine watano ambao tayari walifikishwa mahakamani Agosti 31, 2020 kuwa ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Saxon Building Contaractors Ltd,Rodrick Ndeonasia,aliyekuwa Meneja wa TPA Kigoma,Ajuye Kheri Msese, Ofisa Uhasibu, Herman Ndiboto Shimbe,Mhandisi Mkazi,Jesse Godwin Mpenzile na Afisa Rasilimali Watu, Lusubilo Anosisye Mwakyusa (wote watumishi wa TPA Kigoma). WASOME HAPA

Kwa mujibu wa Mkuu huyo wa TKUKURU mkoani Mwanza, wakati watuhumiwa hao wakifikishwa mahakamani, Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU,Brigedia Jenerali John Mbungo, alitoa taarifa kwa umma ya kutafutwa kwa Madaraka Robert Madaraka ambaye tayari amenaswa juzi na ataunganishwa pamoja na wenzake kwenye mashitaka yanayowakabili.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news