Watanzania waendelea kumuenzi Hayati Dkt.Magufuli, Kada CCM atoa rai



WATANZANIA wameendelea kumuenzi Rais, Dkt. John Magufuli kwa kusema kuwa alikuwa ni mtu wa aina yake na kumuomba Makamu wa Rais Philip Mpango kumsaidia Rais Samia Suluhu Hassan kukamilisha miradi iliyoachwa na Rais huyo, anaripoti Mwandishi DIRAMAKINI.
Hayo yalisemwa Jijini Dar es Salaam jana na Kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM), ambaye pia ni Mjasiriamali, Charles Sabiniani wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Amesema ni wakati mwafaka kwa watanzania kuendelea kumuenzi Rais Magufuli huku wakiendelea kumuunga mkonoj Rais Mama Suluhu kwa utendaji wake na kuepukana na vitendo vya rushwa ambavyo vilimchukiza Hayati.

"Lakini pia namuomba Makam wa Rais ajitahidi kuhakikisha anamsaidia Rais katika kukamilisha miradi iliyoachwa na Hayati," alisema Kada Sabiniani.

Naye Katibu (CCM) Kata ya Ndugumbi Ahmed Said, alisema njia sahihi ya kumuenzi kiongozi huyo ni kufanya kazi kwa juhudi na kudumisha uzalendo wa Taifa.

Alisema kufanya hivyo ni moja ya njia moja wapo ya kumuenzi na kumbuka vyema Hayati Dk. John Magufuli

"Hayati Rais Magufuli alikuwa mzalendo wa kwanza aliyependa nchi yake na kuilinda kwa nguvu zote na kuitetea bila woga," alisema.

Katibu wa Vijana Kata ya Ndugumbi kupitia CCM aliwataka wananchi kufanya kazi kwa juhudi na kujiepusha na vitendo vya Rushwa.

Aidha, aliwataka watanzania kumuunga mkono Rais mteule Samia Suruhu katika majukum yake mapya ya kuliongoza taifa.

"Tuna imani kubwa na Rais Samia kwani alikuwa pamoja na kiongozi wetu Hayati Dk.John Magufuli na amejifunza mambo mengi kutoka kwake," alisema.

Aliwataka watanzania Kuendelea kumeombea kiongozi huyo katika majukum yake hayo mapya iliaweze kuendeleza kasi kama aliyokuwa nayo mtangulizi wake.

"Rais Samia ameanza vyema hivyo tunaamini kabisa ataendelea na kasi hiyo kuhakikisha wanamuenzi Hayati Magufuli," alisema

Hata hivyo alisema viongozi wengine wanatakiwa kuchapa kazi kwa bidii sana ilikutimiliza miradi yote aliyooacha Hayati Magufuli.

"Umoja ni nguvu utengano ni udhaifu watanzania tunie mamoja tushikamane tujiepushe na mizozo na malumbano yasiyo natija tuangalie katika maendeleo zaidi," alisema

Aliwataka viongozi wake dini na watanzania kuwaombea viongozi walioko madarakani ilikuleta weledi zaidi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news