Majambazi yamuua mlinzi akiwa lindoni

Jeshi la polisi Mkoani Simiyu linawashikilia watu watano wanaoudhania kuwa ni majambazi, kwa kosa la wizi na mauaji ambapo wanadaiwa kumuua Peter Ndwani (40) mmasai ambaye alikuwa mlinzi, anaripoti Derick Milton, Simiyu.

Watuhumia hao wanadaiwa kutenda makosa hayo usiku wa kuamkia leo majira ya saa 9:00 alfajiri, baada ya kuvamia nyumbani kwa mfanyabishara wa mjini Bariadi John Sabu eneo la Kidulya halmashauri ya mji wa Bariadi lengo likiwa kuiba gunia za alzeti.
Akizungumza na waandishi wahabari leo ofisini kwake, Kamanda wa Polisi Mkoani hapa Richard Abwao amesema kuwa watuhumiwa hao wakati wakitaka kutekeleza uharifu huo, walikutana na upinzani kutoka kwa marehemu Ndwani ambaye alikuwa mlinzi nyumbani hapo.

Amesema kuwa, mlinzi wakati akipambana nao alizidiwa nguvu, na kupigwa kitu kizito kichwani na kisababisha kifo chake papohapo, na baada ya uchunguzi wa mwili wake alikutwa na majeraha kwenye paji lake la uso.

Amesema, baada ya mauaji hayo watu hao walianza kutekeleza wizi huo, na wakati wakibeba magunia hayo yaliyokuwa yamehifadhiwa ndani ya ghala lililopo nyumbani hapo, ndipo mmoja wa wanafamilia alipowasikia na kupiga kelele.

"Baada ya kupiga kelele, baadhi walikimbia lakini wananchi na wanafamilia walifanikiwa kumkamata mmoja na kuanza kuwataja wenzake, ndipo na wengine wakakamatwa, ndani ya hilo ghala kulikuwemo na gunia 200 za alzeti,"amesema Abwao.

Kamanda Abwao amesema kuwa, jeshi hilo linaendelea na uchunguzi ikiwemo mahojiano na watuhumiwa hao waliokamatwa, na baada ya upelelezi kukamilika watafikishwa mahakamani.

Post a Comment

0 Comments