Mazungumzo ya Rais Samia, Uhuru Kenyatta yafana jijini Nairobi

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 04 Mei, 2021 ameanza Ziara Rasmi ya siku 2 nchini Kenya kufuatia mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Uhuru Muigai Kenyatta, ANARIPOTI MWANDISHI MAALUM DIRAMAKINI.

Baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta Jijini Nairobi, Mhe. Rais amepokelewa rasmi na mwenyeji wake Mhe. Rais Kenyatta katika Ikulu ya Nairobi ambapo amekagua gwaride rasmi lililoandaliwa kwa ajili yake, amepigiwa mizinga 21, amefanya mazungumzo ya faragha na mwenyeji wake na kufuatiwa na mazungumzo rasmi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Rais wa Kenya Uhuru Muigai Kenyatta mara baada ya kuwasili katika Ikulu ya Nairobi nchini Kenya leo Mei 4, 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwa amesimama pamoja na Rais wa Kenya Uhuru Muigai Kenyatta wakati wa nyimbo za Mataifa Mawili ya Tanzania na Kenya zikipigwa mara baada ya kuwasili katika Ikulu ya Nairobi nchini Kenya leo Mei 4, 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akikagua Gwaride la Heshima aliloandaliwa na Jeshi la Ulinzi la Kenya (KDF) mara baada ya kuwasili katika Ikulu ya Nairobi nchini Kenya leo Mei 4, 2021.   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akisaini Kitabu cha Wageni Mara baada ya Kuwasili katika Ikulu ya Nairobi nchini Kenya.

Baadaye viongozi hao wamezungumza na vyombo vya habari ambapo Mhe. Rais Samia amemshukuru Mhe. Rais Kenyatta kwa mwaliko na mapokezi mazuri yaliyopambwa na wananchi waliojitokeza kwa wingi kumlaki wakati akipita barabarani hali inayothibitisha urafiki, udugu na ujirani mwema wa Tanzania na Kenya.

Mhe. Rais Samia amesema pamoja na kuwepo changamoto mbalimbali katika uchumi, Tanzania imedhamiria kukuza zaidi uchumi wake na hivyo kwa kutambua kuwa Kenya ni nchi inayoshika nafasi ya 5 kwa uwekezaji mkubwa nchini Tanzania na nafasi ya 1 Afrika, anawaalika wafanyabiashara na wawekezaji wengi zaidi kutoka Kenya kuwekeza nchini Tanzania kwa manufaa ya pande zote mbili.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwa katika Mazungumzo na Rais wa Kenya Uhuru Muigai Kenyatta mara baada ya kuwasili Nairobi nchini Kenya leo Mei 4, 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akizungumza jambo na Rais wa Kenya Uhuru Muigai Kenyatta wakati wakielekea kwenye mazungumzo ya Pamoja na Ujumbe wa nchi mbili Tanzania na Kenya. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiongoza Ujumbe wa Tanzania katika mazungumzo ya pamoja na Ujumbe wa Kenya uliongozwa na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta leo Mei 4, 2021. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiongoza Ujumbe wa Tanzania katika mazungumzo ya pamoja na Ujumbe wa Kenya uliongozwa na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta leo Mei 4, 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwa na Rais wa Kenya Uhuru Muigai Kenyatta wakati wakishuhudia Mawaziri wa Tanzania (Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula na Waziri wa Michezo wa Kenya Balozi Amina Mohamed wakati wakisaini mkataba wa Mambo ya Sanaa katika Ikulu ya Nairobi nchini Kenya. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwa na Rais wa Kenya Uhuru Muigai Kenyatta wakati wakizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika katika Ikulu ya Nairobi nchini Kenya.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwa amesimama mara baada ya kuweka shada la maua kwenye Kaburi la Hayati Mzee Jomo Kenyatta Rais wa Kwanza wa Kenya lililopo jijini Nairobi nchini Kenya. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Rais wa Kenya Uhuru Muigai Kenyatta mara baada ya mazungumzo yao katika Ikulu ya Nairobi nchini Kenya. (PICHA NA IKULU). 

Amesema, kampuni 513 za Kenya zimewekeza nchini Tanzania mtaji wa Dola za Marekani Bilioni 1.7 (sawa na shilingi za Tanzania Trilioni 3.888) ambazo zimezalisha ajira 51,000 ilihali kampuni 30 za Tanzania.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news