Mkuu wa Mkoa apewa kazi ya kuinusuru Lipuli FC kushuka daraja

Na CATHERINE MBIGILI,Iringa 

MKUU Wa Mkoa wa Iringa,Queen Sendiga ameahidi ndani ya siku mbili kabla ya Jumamosi kukutana na uongozi wa timu ya Lipuli FC ili kuweka mikakati ya namna ya kuinusuru timu hiyo kuendelea kubaki ligi daraja la kwanza.
Timu hiyo inakaribia kushuka nafasi kutoka ligi daraja la kwanza hadi ligi daraja la pili ambapo wamebakiza mechi moja ambayo wakipoteza wapo katika hatari ya kushuka daraja.

Akizungumza wakati wa utambulisho katika ofisi za Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkuu huyo alisema kuna ulazima wa kuisadia timu hiyo kuendelea kubaki licha ya kusalia siku chache ili kucheza mchezo wake wa mwisho.

"Siku zinaonekana zimeisha, lakini siku moja Inaweza kuwa kubwa na ikaleta mabadiliko makubwa na timu ikafanya vizuri,"amesema Queen. 

Amesema, kama uongozi watakutana na kujadiliana masuala ya msingi na kutengeneza mkakati wa muda mfupi ambao utakwenda kuzaa matunda mazuri ili timu iweze kushinda na kuendelea kusonga mbele.
Akiwasilisha mwenendo wa timu hiyo, Katibu wa Chama Cha Mapinduzi, Brown Mwangomale alisema, Iringa ina timu ambayo bado haipo vizuri kutokana na ukata wa kifedha unaoikabili timu hiyo.Alisema, hali ya timu ni mbaya baada ya kushuka ligi kuu lakini haifanyi vizuri hivyo imebakiza mechi moja ambayo wanakwenda kuicheza Jumamosi.

Katibu huyo aliomba kabla ya mechi hiyo kuchezwa kama viongozi wakutane na uongozi wa timu ili kuona kitu gani cha kufanya ili kuisaidia timu kusalia.

Alisema, endapo wangeisaidia mwakani ingerudi ligi kuu na kusaidia vijana kupata ajira na kukuza uchumi wa wana Iringa.

Alisema, watu wa Iringa hawachukulii michezo kama ni ajira na hivyo kutoitilia umakini na msisitizo kama ilivyo kwa mikoa mingine.

"Timu kama Yanga na Simba zinapokuja hapa kwetu zinatumia gharama ambazo wananchi wa Iringa wanajipatia kipato kwa vijana pamoja na wafanyabiashara,"amesema Katibu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news