Rais Samia awatoa hofu wawekezaji nchini Tanzania

Na Diramakini (diramakini@gmail.com).

RAIS Samia Suluhu Hassani amempongeza mfanyabiashara, Alhaji Aliko Dangote ambaye amewekeza katika kiwanda kikubwa cha uzalishaji wa saruji Mkoani Mtwara na amemhakikishia kuwa Serikali itahakikisha uwekezaji wake na wawekezaji wengine unalindwa kwa manufaa ya pande zote mbili.
Ameyasema hayo Ikulu jijini Dar es Salaam alipokuta na kufanya mazungumzo na mfanyabiashara Alhaji Dangote.

Alimpongeza kwa uwekezaji alioufanya hapa nchini na kumuagiza Waziri wa Uwekezaji, Geoffrey Mwambe, Waziri wa Viwanda na Biashara, Prof. Kitila Mkumbo na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Hamad Masauni ambao walihudhuria mazungumzo hayo kufanyia kazi changamoto zote zinazokikabili kiwanda cha Dangote ili kiendelee kuzalisha inavyotakikana na kuleta manufaa yaliyokusudiwa.

Baada ya mazungumzo hayo, Alhaji Dangote alimpongeza Rais Samia kwa kuchukua hatua mbalimbali za kuboresha mazingira ya biashara nchini Tanzania na alimuahidi kuwa kampuni yake ambayo imewekeza hapa nchini kiasi cha Dola za Marekani Milioni 770 (sawa na shilingi Trilioni 1.761) itaendelea kuwekeza katika maeneo mengine ikiwemo mpango wake wa kujenga kiwanda cha kuzalisha mbolea.

“Tutaendelea kuwekeza Tanzania ili kuzalisha ajira, mapato ya nchi na kuinua ustawi wa wananchi wa Tanzania, nadhani anahitaji kuungwa mkono katika hili na tumemuahidi kuwa tutaendelea kuwekeza kwa kiasi kikubwa hapa Tanzania ili kuunga mkono anachokifanya, sisi tutazalisha ajira,”amesema Alhaji Dangote.

Amesema, kutokana na kubadilika na kuimarika kwa mazingira ya biashara nchini Tanzania atawahimiza wafanyabiashara na wawekezaji wenzake kuwekeza Tanzania kwa kuwa Serikali ipo tayari kushirikiana nao.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news