Rais Samia kulihutubia Bunge la Kenya, kufanya ziara ya siku mbili

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan atafanya Ziara Rasmi ya siku 2 katika Jamhuri ya Kenya kuanzia tarehe 04 Mei, 2021 kwa mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Kenya, Mhe. Uhuru Muigai Kenyatta.

Akiwa nchini humo, Mhe. Rais Samia atafanya mazungumzo rasmi na mwenyeji wake Mhe. Rais Kenyatta na kisha atalihutubia Bunge la Kenya litakalojumuisha Wabunge wa Mabunge yote mawili ya nchi hiyo.

Aidha, Mhe. Rais Samia atahudhuria na kuhutubia mkutano wa jukwaa la wafanyabiashara wa Kenya na Tanzania utakaofanyika Jijini Nairobi kwa lengo la kujadiliana masuala mbalimbali yahusuyo fursa za biashara na uwekezaji zilizopo Tanzania na Kenya.

Matukio ya ziara hii yatarushwa mbashara na vyombo vya habari vya redio, televisheni na mitandao ikiwemo youtube channel ya Ikulu Mawasiliano na akaunti rasmi za Instagram, Facebook na Twitter.

Post a Comment

0 Comments