Rais Samia kuzungumza na wazee mkoani Dar es Salaam

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan leo Mei 7, 2021 anatarajia kuzungumza na wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam katika mkutano utakaofanyika ukumbi wa Mlimani City na kuhusisha wazee takribani 900.
Hayo yameelezwa Mei 6, 2021 na mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Abubakar Kunenge ambaye alibainisha kuwa kulikuwa na utaratibu maalum wa kuwapata wazee hao na kwamba wengine wanapaswa kufuatilia mkutano huo kupitia vyombo mbalimbali vya habari.

Kunenge amewaambia waandishi wa habari kuwa, mkutano huo utafanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani City kuanzia saa 8 mchana.

Kunenge ametoa wito kwa Wazee waliopata mwaliko wa kushiriki mkutano huo kujitokeza kwa wingi, ili wapate kusikiliza kile ambacho Rais Samia Suluhu Hassan amewaitia

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news