Magazeti leo Julai 9,2026

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano, Mhe. Deus Sangu, amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Kazi wa Qatar, Mhe. Dkt. Ali bin Samikh Al Marri jana Julai 8, 2026, jijini Doha, nchini Qatar.
Mazungumzo ya Viongozi hao yamelenga kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Qatar katika sekta ya kazi na ajira, hususan eneo la kukuza maendeleo ya rasilimali watu, ulinzi na haki za wafanyakazi pamoja na kuongeza fursa za ajira kwa Watanzania.

Vilevile, wamejadili kuhusu Mkutano wa Uhamaji wa Wafanyakazi (Labour Mobility Dialogue) utakaowakutanisha nchi wanachama wa Baraza la Ushirikiano la Nchi za Ghuba (GCC), Jordan, Lebanon na nchi za Afrika zinazotuma wafanyakazi nje ya nchi chini ya mwamvuli wa Umoja wa Afrika (African Union).

Mkutano huo unatarajiwa kufanyika Oktoba 2026 Tanzania, jijini Dar es Salaam, ukiwa na lengo la kuimarisha ushirikiano, kubadilishana uzoefu na kupanua fursa za ajira salama na zenye staha kwa wananchi wa nchi shiriki.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here