Waziri wa Habari, Michezo, Sanaa na Utamaduni na Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini, Paul Makonda amesema watu wasiokuwa na uwezo wa kifedha katika Jiji la Arusha watapata huduma ya kupima afya bure kila mwaka sambamba na huduma ya matibabu.

Makonda amesema hayo Julai 14 katika kambi ya matibabu Uwanja wa Shekh Amri Abeid na kuratibiwa na ofisi yake.
Amesema mara nyingi utaratibu wa kupima afya hufanywa na watu wenye uwezo wa kifedha lakini hilo litakuwa tofauti kwa wakazi wa jiji hilo.
Makonda amesema Rais Samia Suluhu Hassan ameridhia kutoa madaktari wake bure na hospitali za umma kwenda Jijini Arusha kutoa huduma ya matibabu bure hivyo wananchi wa Jiji la Arusha wanapaswa kuitumia fursa hiyo kikamilifu katika maisha yao ya baadaye.
‘’Madaktari wote bingwa nchini wameitikia wito wa kupiga kambi ya matibabu hapa Arusha hivyo basi nataka kuona kila mkazi wa Jiji la Arusha mwenye changamoto ya afya afike kupata tiba bila malipo,” amesema Makonda.








Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo















