Serikali yataja mikakati kuimarisha uchumi wa Bluu

Na Diramakini (diramakini@gmail.com)

Naibu Waziri wa Wizara ya Uvuvi na Mifugo, Abdalah Ulega amesema Serikali imeweka mkakati kufanikisha uchumi wa Bluu kwa kutumia teknolojia,kwa kuwapa elimu wavuvi kutumia vifaa vya kisasa ili wafanye uvuvi wenye tija.
Kauli hiyo imekuja baada ya swali la nyongeza kutoka kwa Mbunge Faharia, Shomari Hamisi ambaye alitaka kujua mikakati ya Serikali ilivyojipanga kufanikisha na kukuza uchumi wa Blue kwa wavuvi ili kukuza mapatao yao.

Akijibu swali Naibu Waziri Uvuvi na Mifugo Abdalah Ulega amesema,Serikali ya Awamu ya sita imejipanga vyema.

"Mh.Spika Msimamo na mkakati wa awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hasana ni juu ya kutumia vyema fursa ya uchumi wa bluu,na katika kutekekeza jambo hilo Serikali ya awamu ya sita imejipanga vyema,kuhakikisha teknolojia ndio itakayoongoza ili tuweze kutumia raslimali zilizopo katika bahari na maziwa makuu.

"Mheshimiwa Naibu Spika teknolojia hii ninpamoja na kuwasaidia wavuvi waweze kutumia vifaa vya kisasa vitakavyowafikisha katika maeneo yenye samaki kwa urahisi na kwa kutumia garama nafuu na vifaa hivi wizara imepanga watumie GPS, mvuvi anapotoka pwani anapokwenda baharini awe tayari na taarifa wapi samaki wanapatikana ili hiyo iweze kumsaidia kwenye muda na matumizi yake ya mafuta," amesema Mhe.Ulega.

Aidha, Mhe.Ulega ameongeza kuwa Serikali katika kuhakikisha Uchumi wa Blue unawafaidisha vijana na akina mama,Serikali imepanga kununua meli 8 ambapo nne zitakua Tanzania Bara na nne Zanzibar.

"Mheshimiwa Naibu Spika Serikali zote mbili ya jamhuri ya muungano wa Tanzania na Serikali ya mapinduzi wa Zanzibar,kwa kutambua umuhimu wa uchumi wa Blue meli 8 kama alivyozitaja zitanunuliwa na kwa kufanya hivyo mashirika yetu makubwa mawili ya ZAFICO na TAFICO yanafufuliwa,na yatanunua meli mbili kwa kuanzia mwaka wa fedha 2021/2022,ZAFICO inatanunua meli mbili na TAFICO meli mbili,hapa zitapatikana ajira kwa vijana wa kitanzania ambao pia watapewa elimu ya kujiandaa na hiyo fursa kubwa,"amesema Ulega.

Na katika upande wa kilimo,Serikali ina mpango wa maendeleo ya kilimo(Agriculture Sector Development Program) ambayo itakuwa inawaanda vijana kwa ajili ya ufugaji wa Samaki katika maeneo ya bahari

"Tunao mpango wa maendeleo ya kilimo ambao utakwenda sambamba na kutengeneza na kuwaanda vijana wetu,ikiwa ni pamoja na shughuli nzima za ufugaji wa samaki katika maeneo ya bahari,tunaita Mariculture ambapo vijana zaidi ya 1000 zanziba na kina mama zaidi ya 15000 watanzania na mradi huu wa AFDP,"amesema Mheshimiwa Ulega.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news