CCM:Tumedhamiria kukuza, kuimarisha na kushamirisha Demokrasia nchini

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka leo Juni 4, 2021 amemuwakilisha Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo katika kikao maalum cha Makatibu Wakuu wa vyama vyote vya siasa vyenye usajili wa kudumu na Msajili wa vyama vyama siasa nchini, Jaji Francis Mutungi.

Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa mikutano wa Samuel Sita uliopo ofisi za Bunge Barabara ya Shaban Robert jijiini Ilala, Dar es salaam.
Shaka amesema, Chama Cha Mapinduzi kimedhamiria kukuza, kuimarisha na kushamirisha Demokrasia nchini.

"Ni kwa kuhakikisha mazingira bora ya kuendeleza siasa safi yanakuwepo kama ambavyo Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hasaan anavyosisitiza nyakati zote kuwa ni muda wa kushikamana bila kujali itikadi zetu kwa maslahi mapana ya Taifa,"amesema Shaka.

Post a Comment

0 Comments