Magazeti leo Machi 8,2026

RAIS wa Uganda, Yoweri Museveni, ameteuliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kwa kipindi cha mwaka mmoja katika mkutano wa 25 wa kawaida wa Wakuu wa Nchi wa jumuiya hiyo.
Akikabidhi uenyekiti huo, Rais wa Kenya, William Ruto, amesema Museveni atachukua nafasi hiyo baada ya yeye kumaliza muda wake wa kuliongoza baraza hilo kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Baada ya kutangazwa, Rais Museveni amemshukuru Rais Ruto kwa kuiongoza jumuiya hiyo katika kipindi cha mwaka uliopita na kuahidi kuendeleza ushirikiano ili kuimarisha maendeleo ya kisiasa, kiuchumi na kijamii ndani ya jumuiya hiyo.

Aidha,ametoa shukrani kwa Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, kwa mapokezi mazuri waliyopata wakati wa mkutano huo uliofanyika jijini Arusha.










Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here