MAKACHERO WAMSHIKILIA MWANAMKE KWA KOSA LA WIZI WA MTOTO


TAREHE 31.05.2021 MAJIRA YA 23:30HRS KATIKA MAENEO KISHIRI, WILAYANI NYAMAGANA, BAADA YA MSAKO MKALI NA UFUATILIAJI WA KINA KWA KUSHIRIKISHA KIKOSI KAZI CHA SAYANSI YA UCHUNGUZI LILIFANIKIWA KUMKAMATA MWANAMKE MMOJA AITWAYE ANASTAZIA KIMARIO, MIAKA 28, MCHAGA, MKAZI WA IGOMA, KWA KOSA LA WIZI WA MTOTO JINSIA YA KIKE, MWENYE UMRI WA WIKI TATU, AMBAYE ALIMWIBA TAREHE 30.05.2021 MAJIRA YA 11:30HRS NYUMBANI KWA MLOKOZI LEOBARD @ MIBAZI HUKO MAENEO YA BUTINDO, KATA YA SHIBULA, WILAYANI ILEMELA.

INADAIWA KUWA MTUHUMIWA ALIKUA AKIPITIA MANYANYASO KWENYE NDOA YAKE HASA UPANDE WA NDUGU WA MUME KWA KUKOSA MTOTO, NDIPO ALIFIKA NYUMBANI KWA BWANA MLOKOZI AMBAYE MKEWE AMEJIFUNGUA HIVI KARIBUNI NA KUANZA KUMSAIDIA MZAZI KAZI NDOGONDOGO AKIJIFANYA NI MTU MWEMA MWENYE HURUMA NA BAADAE KUPATA FURSA YA KUMUIBA MTOTO WAKATI MAMA YAKE AKIWA ANAFUA NJE YA NYUMBA . 
 
JESHI LA POLISI LINAMALIZIA UPELELEZI WA SHAURI HILI NA MTUHUMIWA ATAFIKISHWA MAHAKAMANI HARAKA IWEZEKANAVYO KWANI KOSA ALILOLITENDA NI MIONGONI MWA MAKOSA MAKUBWA YA KIJINAI .

JESHI LA POLISI LINATOA WITO KWA WANANCHI HASA WANAWAKE WENYE CHANGAMOTO ZA KUKOSA WATOTO WAENDE HOSPITALI NA KUWASHIRIKISHA WATAALAMU WA TIBA ZA WANAWAKE ILI KUTATUA CHANGAMOTO HIZO . PIA LINAWASIHI WANAUME KUACHA TABIA ZA KUWANYANYASA WANAWAKE WENYE CHANGAMOTO HIZO KWANI WAKIPEANA USHIRIKIANO WA KIMATIBABU CHANGAMOTO HIZI ZINAWEZA KUTATULIWA. 
 
JESHI LA POLISI LINAWASHUKURU WANANDHI WOTE WAKIWEMO WAANDISHI WA HABARI KWA KUFANYA KAZI KAMA MBWA WANAOBWEKA (WATCH DOG) NA KUWEZESHA TAASISI ZA UMMA WAKIWEMO WASIMAMIZI WA SHERIA KAMA JESHI LA POLISI KUFANYA KAZI KWA HAKI HUKU WAKIZINGATIA SHERIA NA KANUNI ZA KAZI.

Post a Comment

0 Comments