Makamu wa Rais atoa maagizo,wito kwa wafanyabiashara, wadau wa mazingira

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango amewataka wafanyabiashara hasa wa gesi ya kupikia majumbani kubuni mbinu za kuwasaidia wananchi wenye kipato cha chini ili waweze kumudu gharama za nishati hiyo mbadala.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango,akizungumza wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya mazingira Duniani iliyoambatana na uzinduzi wa kampeni kabambe ya Kitaifa ya usafi na usimamizi wa mazingira nchini iliyofanyika Juni 5,2021 jijini Dodoma.

Ameyasema hayo Juni 5, 2021 katika maadhimisho ya siku ya mazingira duniani yaliyofanyika kitaifa jijini Dodoma.

Dkt.Mpango amesema, licha ya uwepo wa baadhi ya nishati mbadala ambazo watu huweza kuzitumia kama vyanzo vya kupikia lakini ukuaji wa matumizi wa nishati hizo ni wa asilimia mbili tu kwa mwaka.

“Tatizo kubwa lililo mbele yetu ni namna gani unapunguza bei ya nishati mbadala na bei ya majiko, sasa naomba niwasihi vyuo vyetu na vinginevyo, watafiti ni nini kinasababisha bei ya nishati mbadala na vifaa husika kuwa kubwa na nini kifanyike.

“Kama ni kuangalia mfumo wa kozi basi tuutazame lakini pia kama ni gharama za kuzalisha nishati mbadala nazo ziweze kutazamwa,” amesema Dkt.Mpango.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Selemani Jafo, akizungumza wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya mazingira Duniani iliyoambatana na uzinduzi wa kampeni kabambe ya Kitaifa ya usafi na usimamizi wa mazingira nchini iliyofanyika Juni 5,2021 jijini Dodoma.

Dkt.Mpango amesema, Serikali, wadau wa maendeleo na asasi za kiraia na sekta binafsi hazina budi kuelekeza nguvu zaidi katika kutekeleza miradi inayolenga kuongeza matumizi ya nishati mbadala ya kupikia ikiwemo gesi, matumizi ya umeme wa jua, matumizi ya majiko banifu na vifaa vinavyotumia nishati kidogo katika kupika.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Marry Maganga, akizungumza wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya mazingira Duniani iliyoambatana na uzinduzi wa kampeni kabambe ya Kitaifa ya usafi na usimamizi wa mazingira nchini iliyofanyika Juni 5,2021 jijini Dodoma.

Amesema, mamlaka husika ikiwemo Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Ofisi ya Makamu wa Rais, Wizara ya Maliasili na Utalii, Wizara ya Nishati na wadau wa maendeleo wanapaswa kubuni na kutekeleza mikakati ya kuongeza utumiaji wa nishati mbadala kwa gharama nafuu.

Amesema, Serikali inaedelea kuteleza mradi wa Ujenzi wa Bwawa la Mwalimu Nyerere huko Rufiji ili kuongeza uzalishaji na upatikanaji wa nishati ya umeme ambapo kukamilika kwa mradi kutasaidia kupunguza gharama ya matumizi ya mkaa.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Antony Mtaka,akizungumza wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya mazingira Duniani iliyoambatana na uzinduzi wa kampeni kabambe ya Kitaifa ya usafi na usimamizi wa mazingira nchini iliyofanyika Juni 5,2021 jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge, Mazingira, Viwanda na Biashara, David Mwakiposa,akizungumza wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya mazingira Duniani iliyoambatana na uzinduzi wa kampeni kabambe ya Kitaifa ya usafi na usimamizi wa mazingira nchini iliyofanyika Juni 5,2021 jijini Dodoma.

Mfanikio ya mradi huo amesema, inategemea upatikanaji wa miti kwenye bonde la mto Rufiji, hivyo wakuu wa mikoa na viongozi wa mamlaka ya serikali za mitaa wanapaswa kuzingatia matumizi ya rasilimali ya maji kwa njia endelevu.

"Nchi imeendelea kukumbwa na athari za mabadiliko ya tabia nchi kama ukame mafurikio, magonjwa ongezeko la kina na kuchangia ongezeko la majanga ya asili kwa nchi zinazoendelea.
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira, (UNEP) Clara Makenya,akizungumza wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya mazingira Duniani iliyoambatana na uzinduzi wa kampeni kabambe ya Kitaifa ya usafi na usimamizi wa mazingira nchini iliyofanyika Juni 5,2021 jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Kamati Maalumu ya Uratibu wa Kampeni ya Mazingira Nchini, Seif Ali Seif,akizungumza wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya mazingira Duniani iliyoambatana na uzinduzi wa kampeni kabambe ya Kitaifa ya usafi na usimamizi wa mazingira nchini iliyofanyika Juni 5,2021 jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Mabalozi wa Kampeni ya Utunzaji Mazingira, Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mussa Salum,akizungumza wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya mazingira Duniani iliyoambatana na uzinduzi wa kampeni kabambe ya Kitaifa ya usafi na usimamizi wa mazingira nchini iliyofanyika Juni 5,2021 jijini Dodoma.

Ametoa rai kwa wizara, taasisi za serikali na wadau kuelimisha wananchi kuhusu mkakati huo.

"Uharibifu mazingira ni dhuluma na ukatili kwa vizazi vijavyo, Serikali ya Awamu ya Sita hatutavumilia kuona dhuluma hiyo ikiendelea,"amesema Dkt.Mpango.
"Serikali itahakikisha waharifu wote wa mazingira wanachukuliwa hatua kali za kisheria. Kamoeni itawawezesha wananchi kufahamu kutunza na kuhifadhi mazingira na kuongeza uwajibikaji kwa watendaji katika kusimamia utunzaji mazingira,"amesema.

Amemtaka Waziri Jafo kusimamia kampeni hiyo siku kwa siku na kuhakikisha inafanikiwa.

"Kampeni umeianzisha mwenyewe na utapimwa na mafanikio ya hiyo kampeni. Ile miti iliyopandwa siku ya matembezi uhakikishe haifi na mimi nitaikagua,"ameagiza Dkt.Mpango.
Baadhi ya washiriki wakifutilia hotuba mbalimbali wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya mazingira Duniani iliyoambatana na uzinduzi wa kampeni kabambe ya Kitaifa ya usafi na usimamizi wa mazingira nchini iliyofanyika Juni 5,2021 jijini Dodoma.
Kwaya ya Chuo cha Utumishi wa Umma Dar es salaam wakitoa burudani wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya mazingira Duniani iliyoambatana na uzinduzi wa kampeni kabambe ya Kitaifa ya usafi na usimamizi wa mazingira nchini iliyofanyika leo Juni 5,2021 jijini Dodoma.
Baadhi ya Wanafunzi wakifutilia hotuba mbalimbali wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya mazingira Duniani iliyoambatana na uzinduzi wa kampeni kabambe ya Kitaifa ya usafi na usimamizi wa mazingira nchini iliyofanyika Juni 5,2021 jijini Dodoma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango akikata utepe kuzindua andiko la kampeni kabambe ya kitaifa ya uhifadhi na usafi wa mazingira kwenye maadhimisho ya siku ya mazingira Duniani iliyoambatana na uzinduzi wa kampeni kabambe ya Kitaifa ya usafi na usimamizi wa mazingira nchini iliyofanyika Juni 5,2021 jijini Dodoma.

"Kila kaya ikapande miti katika maeneo yao,kuelimisha umma kuachana na mila potofu zinazoharibu miti na misitu. Halmashauri zikasimamie na kudhibiti uharibu mazingira kwa sababu ya wivu, uonevu au imani potofu," amesema.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Philip Mpango akionyesha andiko la kampeni kabambe ya kitaifa ya uhifadhi na usafi wa mazingira kwenye maadhimisho ya siku ya mazingira Duniani iliyoambatana na uzinduzi wa kampeni kabambe ya Kitaifa ya usafi na usimamizi wa mazingira nchini iliyofanyika Juni 5,2021 jijini Dodoma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango akibonyeza kitufe akizindua Mfumo wa Kielektroniki wa Usimamizi wa Kampeni Kabambe ya Usafi Nchini kwenye maadhimisho ya siku ya mazingira Duniani iliyoambatana na uzinduzi wa kampeni kabambe ya Kitaifa ya usafi na usimamizi wa mazingira nchini iliyofanyika Juni 5,2021 jijini Dodoma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akimkabidhi Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Bi Mary Maganga andiko la kampeni kabambe ya kitaifa ya uhifadhi na usafi wa mazingira kwenye maadhimisho ya siku ya mazingira Duniani iliyoambatana na uzinduzi wa kampeni kabambe ya Kitaifa ya usafi na usimamizi wa mazingira nchini iliyofanyika Juni 5,2021 jijini Dodoma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango, akimsikiliza Msanii Mai Zumo,maadhimisho ya siku ya mazingira Duniani iliyoambatana na uzinduzi wa kampeni kabambe ya Kitaifa ya usafi na usimamizi wa mazingira nchini iliyofanyika Juni 5,2021 jijini Dodoma.

"Wafugaji waache kuchunga ndani ya mashamba ya mazao ya miti, kukata miti kwenye hifadhi, Serikali za Vijiji ziwajibike kutunza misitu ya asili katika maeneo yao na kusimamia sheria ndogo za utunzaji mazingira.


"Kila Mkuu wa mkoa na katibu tawala miti wapande miti milioni 1.5 kwa mwaka, zamu hii tutakaguana, ahakikishe na kufuatilia kuona miti iliyopandwa inatunzwa na kukua,"amesema.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango, akiangalia baadhi ya Matumizi ya Nishati Mbadala kuongoa Mifumo Ikolojia,alipotembelea banda la Umoja wa Mataifa kwenye maonyesho ya maadhimisho ya siku ya mazingira Duniani.

Post a Comment

0 Comments