Mbunge Sanga alia na Serikali ujenzi Kituo cha afya Ikuwo

Na Doreen Aloyce, Diramakini Blog

Naibu waziri wa Nchi Ofsi ya Rais -TAMISEMI, Festo Ndugage amesema ili kuboresha huduma za afya katika Wilaya ya Makete Serikali imeipatia Halmashauri ya Wilaya ya Makete Shilingi milioni 400 katika mwaka wa fedha 2017/18 kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya Ipele.
Kauli hiyo ameitoa Bungeni Dodoma wakati alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Makete, Festo Sanga alipouliza swali je,ni lini Serikali itaanza ujenzi wa kituo Cha Afya Ikuwo.

Naibu Waziri huyo amesema, ujenzi wa kituo hicho cha Ipele umekamilika na kinatoa huduma zikiwemo huduma za dharura za upasuaji.

Aidha, ameongeza katika mwaka wa fedha 2020/21 Serikali imeipatia Halmashauri ya Wilaya ya Makete shilingi milioni 150 kwa ajili ya ukamilishaji wa Zahanati za Usungilo, Nungu na Matenga.

Amesema kuwa, mwezi Mei 2021 Serikali iliipatia Halmashauri ya Wilaya ya Makete Shilingi milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya Kitulo.

"Nikutoe wasiwasi Mheshimiwa Mbunge ombi la kituo cha afya Ikuwo limepokelewa na linafanyiwa tathimini Serikali inaipitia na kuiboresha sera ya ujenzi wa zahanati kila Kijiji na kituo cha afya kila kata ili ujenzi ufanyike kimkakati na kwa tija zaidi badala ya kila kijiji na kila Kata,"amesema Ndugage.

Mbunge Festo Sanga amesema kuwa kutokuwepo kwa kituo hicho kunapelekea wananchi wake kutembea zaidi ya kilometa 70 kufikia hospital ya Wilaya.

Amesema kuwa, adha hiyo imekuwa ikileta madhara kwani wajawazito wanajifungulia njiani ,na wengine upoteza maisha kwa ajili ya umbali kwani hawapati matibabu kwa wakati.

Ameiomba Serikali kuangalia suala hilo kwa jicho la pili ili kuweza kunusuru maisha ya watu na kuepuka vifo visivyo vya lazima.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news