Magazeti leo Februari 18,2026

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imezindua Kituo cha Huduma kwa Walipa Kodi Masaki jijini Dar es Salaam, hatua inayolenga kusogeza huduma karibu na wafanyabiashara na kuongeza ufanisi wa ukusanyaji wa mapato ya Serikali.
Kituo hicho kinatarajiwa kurahisisha usajili, ulipaji na upatikanaji wa elimu ya kodi kwa wafanyabiashara wa Masaki, Oysterbay na Msasani, maeneo yenye shughuli nyingi za kiuchumi na uwekezaji mkubwa wa sekta binafsi.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Kamishna Mkuu wa TRA, Yusuph Mwenda, amesema uwepo wa kituo hicho ni sehemu ya mkakati wa kuimarisha huduma na kupanua wigo wa walipa kodi katika eneo lenye wafanyabiashara wa kipato cha kati na juu.
Amesisitiza matumizi ya mifumo ya kidijitali katika utoaji wa huduma, akieleza kuwa hatua hiyo itarahisisha taratibu, kupunguza gharama kwa walipa kodi na kuongeza usawa wa kikodi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here