Muongozo wa DPP mpya kuamua hatima ya kesi ya Herbinder Seth, Rugemarila

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Juni 3, 2021 upande wa mashtaka, umeileza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu iliyopo Jiji la Ilala mkoani Dar es Salaam kuwa, mazungumzo ya makubaliano ya kumaliza kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili Mkurugenzi wa Kampuni ya Kufua Umeme (IPTL), Herbinder Seth yanasuburi muongozo wa Mkurugenzi mpya wa Mashtaka nchini (DPP),Sylvester Mwakitalu.

Wankyo Simon ambaye ni Wakili wa Serikali Mwandamizi amedai hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi wakati kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kutajwa na kuangalia hatua ya mazungumzo na upelelezi ulipofikia.

Amedai kuwa,mazunguzo ya kumaliza kesi dhidi ya mshtakiwa ( Herbinder Seth) yanaendelea yalipoishia.

"Hivyo, tunasuburi muongozo kutoka kwa DPP mpya aliyeteuliwa hivi karibuni na Rais ili tuweze kuwasilisha mahakamani hapa,"alidai Wakili Wankyo huku akieleza kuwa,upande wa mawakili wa Seth waendelee kufuatilia kwa hatua zinazoendelea.

Awali Seth na Wakili wa Kujitegemea Joseph Makandege waliwasilisha ombi kwa DPP wakionesha nia yao ya kutaka maliza kesi kwa kukiri makosa yao, lakini, Mei 6,mwaka huu, Wakili huyo aliondoa nia yake ya kufanya makubaliano na DPP akieleza kwamba mazungumzo hayo yamechukua muda mrefu kukamilika.

Mbali na Seth na Makandegs mshtakiwa mwingine ni mfanyabiashara James Rugemalira ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya VIP, wanadaiwa kutenda makosa hayo katika Jiji la Dar es Salaam na nchi za Afrika Kusini, Kenya na India.

Washtakiwa wanakabiliwa na mashtaka 12 yakiwemo ya utakatishaji fedha, miongoni mwa mashtaka hayo yapo ya kula njama, kujihusisha mtandao wa uhalifu, kughushi na kutoa nyaraka za kughushi na kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu, kutakatisha fedha na kusababisha hasara ya Dola za Marekani 22,198,544.60 na Sh 309,461,300,158.27.

Washtakiwa wanadaiwa kati ya Oktoba 18 ,2011 na Machi 19, 2014 jiji Dar es Salaam walikula njama katika nchi za Afrika Kusini, Kenya na India ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Kwa upande wake Mwanasheria Joseph Makandege anakabiliwa na mashtaka matano likiwemo la kuisababishia Serikali hasara ya Dola za Marekani laki tisa na themanini.

Post a Comment

0 Comments