Rais Samia awaacha kando Lengai Ole Sabaya, Kasesela na Simon Odunga

Na Mwandishi Diramakini

Katika uteuzi huo ambao umefanyika leo Juni 19, 2021 aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya ameachwa kando.
Mei 13, 2021 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan alimsimamisha kazi, Lengai Ole Sabaya ili kupisha uchunguzi wa tuhuma mbalimbali zinazomkabili.

Wengine walioachwa katika uteuzi huo ni pamoja na Simon Odunga ambaye alikuwa mkuu wa Wilaya ya Rorya mkoani Mara.

Sambamba na aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Iringa mkoani Iringa, Richard Kasesela.

Post a Comment

0 Comments