Rais Samia awateua Wanahabari watano ukuu wa Wilaya

Na Mwandishi Diramakini

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan leo Juni 19, 2021 ameteua wakuu wa Wilaya mbalimbali wakiwemo wanahabari.
Simon Simalenga wa Clouds Media Group

Katika uteuzi huo, Rais Samia amewateua waandishi wa habari kushika nafasi hiyo.

Walioteuliwa ni Fatma Almas Nyangasa wa Azam TV (Kigamboni), Simon Simalenga wa Clouds Media Group (Songwe) na Abdallah Mwaipaya wa ITV/Radio One (Mwanga).

Gabriel Zakaria Olemegili kutoka TBC kuwa Mkuu wa Wilaya ya Busega na Mohamed Ngoma kutoka Clouds Media  amemteua kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Mkoani Lindi, kabla ya uteuzi huo Ngoma alikuwa DAS Singida.

Wakuu wa Wilaya wateule wataapishwa kuanzia tarehe 21 Juni, 2021 saa nne (4) asubuhi na Wakuu wa Mikoa yao.

Post a Comment

0 Comments