RC Dkt.Sengati aonya watumishi watakaozorotesha maendeleo Shinyanga

Na Anthony Ishengoma,Shinyanga

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati amesema hatakuwa mvumilivu kwa viongozi na watumishi wa umma watakaoshindwa kusimamia na kusababisha kuzorota kwa maendeleo ndani ya Mkoa wa Shinyanga.

Dkt. Sengati alisema hayo jana wakati akiwakaribisha viongozi Wakuu wa Wilaya wapya wa Wilaya za Kishapu na Kahama waliofika katika Ofisi za Mkuu wa Mkoa kujitambulisha mbele yake lakini pia pia mbele ya wadau mbalimbali wa walioko mkoa wa Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga katikati akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wapya wa Wilaya waliofika ofisini kwake jana kwa lengo la kujitambulisha na kuanza kazi katika vituo vyao vipya vya kazi.

‘’Sitavumilia, nitahakikisha natumia mbinu zote kuhakikisha wanachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria taratibu na kanuni za kiutumishi lakini pia hatua za kinidhamu kwasababu watanzania ni wengi wenye uwezo wa kuwahudumia wananchi.’’Alisisitiza Dkt. Sengati Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.

Aidha Dkt. Sengati aliwataka Wakuu wa Wilaya wapya kufanya tathimini ya kina ili kuja na mikakati ya kuendeleza Shinyanga kama mkoa wa kimkakati na inayoendana na Tanzania ya uchumi wa kati lakini pia ulimwengu wa kidijitali ili kudhibitisha kuwa wao ni viongozi wa karne hii ya Sayansi ya na Teknolojia.

‘’Napenda kuona mahusiano makubwa ya utajiri wa Mkoa wetu na ubora wa maisha ya wana Shinyanga, natamani kilimo,madini na mifugo takribani milioni nne, biashara kubwa na uwekezaji ulioko Shinyanga uhakisiwe katika ubora wa maisha ya watu wa Shinyanga.’’ Alisisitiza Dkt. Sengati.

Sehemu ya wadau wa Mkoa wa Shinyanga waliofika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga kushiriki makaribisho ya Wakuu wa Wilaya wapya wa Wilaya zinazounda Mkoa wa Shinyanga.




Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati akiongea na wadau wa Mkoa wa Shinyanga waliofika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga kushiriki makaribisho ya Wakuu wa Wilaya wapya wa Wilaya zinazounda Mkoa wa Shinyanga.

‘’Unapomwondoa mtu katika umasikini maana yake unataka naye awe sehemu ya nguvu ya soko na awe na uwezo wa kununua na hivyo aweze kuchangia katika ujenzi wa uchumi tunataka Kahama inayokuwa na nguvu kubwa ambayo kila mmoja anaweza kuingia sokoni. Hivi karibuni Serikali ya awamu ya Sita imefanya mabadiliko katika uongozi wa Wilaya mbalimbali nchini na katika mabadiliko hayo Mkoa wa Shinyanga ulibata madiliko ya viongozi hao kwa Wilaya zake mbili za Kishapu pamoja na Kahama.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here