MAKUMBUSHO ya Taifa imetangaza shindano la kizalendo la kuimba wimbo wa Taifa “Tanzania Tanzania”, linalolenga kuhamasisha uzalendo, kudumisha utambulisho wa Taifa, na kuitangaza Makumbusho ya Taifa, ambapo mshindi wa shindano hilo atajipatia zawadi ya Shilingi 5,000,000.
Shindano hilo limeandaliwa kutokana na changamoto ya ukosefu wa uelewa wa jamii kuhusu Makumbusho ya Taifa na malengo yake. Shindano hilo linafungua fursa kwa mtu yeyote mwenye sauti ya kuvutia, hususan wanamuziki wenye ujuzi, kushiriki kwa kuongeza ubunifu na hisia katika kuimba wimbo huo.
Washiriki wanatakiwa kufuata taratibu maalum katika kuwasilisha wimbo wao. Miongoni mwa masharti ni kuandaa video itakayokuwa na utambulisho wa mshiriki na kutaja watu wa tatu, mshiriki anatakiwa kuvaa vazi la kizalendo lenye rangi za bendera ya Tanzania au vazi lolote la asili litakaloakisi utamaduni wa Tanzania, kama vile kitenge au batiki.
Vigezo vingine vya kushiriki ni kurekodi sauti na video zenye ubora wa hali ya juu zisizozidi dakika mbili. Washiriki pia wanashauriwa kutumia hashtags maalum zitakazorahisisha ufuatiliaji wa wimbo wao, zikiwemo: #Tumerithishwa #Tuwarithishe #UrithiWetu #FahariYetu #MuseumsTZ #KaziNaUtuTunasongaMbele.
Shindano hili lililoanza Februari 10 hadi Machi 20, 2026 linatarajiwa kuongeza uelewa wa Watanzania kuhusu historia, utamaduni, na umuhimu wa Makumbusho ya Taifa, huku likiwahamasisha kuwa mabalozi wa uzalendo kupitia muziki.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo





.jpg)





