SIMIYU NA SONGWE WAANZA KWA KISHINDO UMITASHUMTA

Na Mathew Kwembe, Mtwara

Mikoa ya Simiyu na Songwe imeanza kwa kishindo katika michuano ya UMITASHUMTA iliyoanza katika viwanja mbalimbali hapa Mtwara baada ya timu zao za soka wavulana kuzifunga bila huruma timu kutoka mikoa ya Arusha na Kilimanjaro.

Timu ya Simiyu iliifunga Arusha kwa magoli 4-0, huku Songwe ikiichabanga Kilimanjaro magoli 4-2.

Morogoro ilifungwa na Mbeya magoli 3-1, Shinyanga iliifunga Mwanza 1-0, Mtwara ikailaza Njombe 2-0 na Kigoma ikatoka sare na Lindi kwa kufungana magoli 2-2 na katika soka wasichana timu ya soka ya mkoa wa Lindi iliifunga Kilimanjaro magoli 2-0.
Kwa upande wa mchezo wa soka maalum uliochezwa kati ya Shinyanga na Kagera, Shinyanga walishinda magoli 5-0.

Matokeo ya michezo ya netiboli iliyochezwa jana jioni inaonyesha kuwa Lindi iliifunga Iringa 14-8, Tabora ilipata magoli 27 dhidi ya 10 ya timu ya mkoa wa Njombe, Dar es salaam ilichabangwa na Tanga kwa magoli 34-17 na Simiyu ikaifunga Arusha 18-13.

Katika mchezo wa goli wavulana Rukwa iliifunga Lindi 10-9, Tabora ikaichapa Shinyanga 22-4, Dodoma ikailaza Tanga 15-12 huku Kilimanjaro ikifungwa na Iringa kwa magoli 10-12.
Matokeo ya mchezo wa wavu kwa upande wa wavulana Ruvuma ilifungwa na Mbeya kwa seti 3-0, Mtwara ikaichapa Manyara seti 3-0, Dar es salaam ikaichalaza Lindi seti 3-0 huku Mara ikiifunga Geita seti 3-1.

Kwa upande wa matokeo ya mpira wa mikono wavulana Mara imeichapa Singida magoli 21-16, Mtwara imefungwa na Morogoro magoli 17-5 na Kilimanjaro imeibugiza Kigoma magoli 14-6.

Matokeo ya mpira wa mikono wasichana Morogoro imeifunga Manyara magoli 12-8 huku timu ya wasichana ya mpira wa mikono kutoka mkoa wa Mara ikiifunga Dodoma kwa magoli 10-6

Kwa mujibu wa Mratibu wa mashindano hayo Leonard Thadeo, michezo hii itachezwa katika hatua za makundi hadi tarehe 14/06/2021.

Michezo ya hatua ya Robo fainali itachezwa tarehe 15/6/2021, na fainali za michuano hiyo itafanyika tarehe 18/6/2021.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news