TAKUKURU:JIEPUSHENI NA MATAPELI

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imeeleza kuwa, kumejitokeza tabia ya baadhi ya watu kujifanya kuwa wao ni MADALALI kati ya jamii na taasisi hiyo.

"Kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Kamishna wa Polisi Salum Hamduni, napenda kutumia fursa hii kutoa taarifa kwa umma kuwa hivi karibuni, kumejitokeza tabia ya baadhi ya watu kujifanya kuwa wao ni MADALALI kati ya jamii na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa - TAKUKURU,"ameeleza Mkuu wa Kitengo Cha Mawasiliano Serikalini- TAKUKURU, DOREEN J. KAPWANI leo Juni 5,2021.

Watu hawa wamekuwa wakiwarubuni baadhi ya wananchi wakiwemo watumishi wa umma kwamba wana uwezo wa kuwapangia ratiba za kuonana au kuwasiliana na Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU na kwamba, kwa kuwa wageni wanaohitaji huduma hii wako wengi, wao wanaweza kuwasaidia kuonana na Mkurugenzi Mkuu kwa haraka.

Wapo wengine wanaowapigia baadhi ya watumishi wa umma na kujitambulisha kuwa wao ni Afisa Habari au Maafisa wa TAKUKURU wakiwataka watu hao waonane nao kwa ajili ya mahojiano.

TAKUKURU inatumia fursa hii kuuleza umma kuwa MADALALI hao ni MATAPELI. Pia, tunawapongeza wananchi wote walioweza kubaini kuwa watu hao ni MATAPELI na wakatoa taarifa TAKUKURU mara moja.

Ifahamike, TAKUKURU ina utaratibu maalumu wa kuwasiliana au kuwaita watuhumiwa au mashahidi ofisini. Utaratibu huu unahusisha kutuma hati ya wito (samansi) kufika Ofisi za TAKUKURU na kuujulisha uongozi wa mhusika kwa maandishi iwapo ni mwajiriwa kama ilivyo utaratibu wa mawasiliano ya ofisi za Serikali. Pia, wakati mwingine hupiga simu ya wito kwa mhusika kufika ofisini na huwa tunajitambulisha kwa utaratibu maalum.

Hivyo, iwapo mwananchi utakuwa na wasiwasi na mtu yeyote aliyekupigia simu, tafadhali jiridhishe kwa kuwasiliana nasi BURE kupitia huduma ya nambari ya simu ya dharura namba MIA MOJA KUMI NA TATU (113) inayopatikana saa 24 kila siku. Lakini pia unaweza kutuma barua pepe kwenda dgeneral@pccb.go.tz.

Vilevile, unaweza kueleza wasiwasi wako juu ya wito ulioupata bila kusahau kututajia namba ya simu ya mtu aliyekupigia kwa kupiga simu nambari 0738150100 au 0738150046; au piga simu kwa Mkuu wa TAKUKURU katika mkoa uliopo. Nambari za simu za Wakuu wa TAKUKURU mikoa ni zifuatazo:

RBC Arusha 0738 150063

RBC Dodoma 0738 150070

RBC Geita 0738 150078

RBC Ilala 0738 150234

RBC Iringa 0738 150084

RBC Kagera 0738 150088

RBC Katavi 0738 150096

RBC Kigoma 0738 150103

RBC Kilimanjaro 0738 150110

RBC Kinondoni 0738 150236

RBC Lindi 0738 150118

RBC Manyara 0738 150124

RBC Mara 0738 150130

RBC Mbeya 0738 150137

RBC Morogoro 0738 150143

RBC Mtwara 0738 150156

RBC Mwanza 0738 150162

RBC Njombe 0738 150170

RBC Pwani 0738 150176

RBC Rukwa 0738 150186

RBC Ruvuma 0738 150190

RBC Shinyanga 0738 150196

RBC Simiyu 0738 150202

RBC Singida 0738 150208

RBC Songwe 0738 150214

RBC Tabora 0738 150218

RBC Tanga 0738 150225

RBC Temeke 0738 150239

Tunaendelea kusisitiza kwenu wananchi, kamwe msikubali kutapeliwa kwani TAKUKURU ni chombo cha Serikali kinachotekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na Taratibu zote za Serikali. Ukiwa na wasiwasi, tafadhali wasiliana nasi kwa namba tulizozitaja.

Mwananchi yeyote anayehitaji huduma ya TAKUKURU tafadhali afike katika ofisi ya TAKUKURU iliyopo karibu naye. TAKUKURU ina ofisi katika kila mkoa na katika kila wilaya Tanzania Bara.

Kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, natumia fursa hii pia kutoa ONYO kwa wale wote wanaojihusisha na UTAPELI au UDALALI huu kwamba tayari namba zao za simu tunazo na zinashughulikiwa ili hatua za kisheria zichukuliwe.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news