Yaliyojiri wakati wa majadiliano ya hotuba ya bajeti Wizara ya Maliasili na Utalii 221/2022
Hotuba ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Mheshimiwa Dkt. Damas Daniel Ndumbaro (MB.), wakati akiwasilisha Bungeni Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022. "Mheshimiwa Spika,ninaomba Bunge lako Tukufu liidhinishe jumla ya Shilingi 571,632,424,000 kwa matumizi ya Fungu 69 -Wizara ya Maliasili na Utalii kwa mwaka wa fedha 2021/2022. 

Kati ya fedha hizo, Shilingi 418,859,544,000 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na Shilingi 152,772,880,000 ni za miradi ya maendeleo. 

Mheshimiwa Spika,fedha za matumizi ya kawaida zinajumuisha Shilingi 153,537,684,000 za mishahara na Shilingi 265,321,860,000 za matumizi mengineyo. Aidha,fedha za miradi ya maendeleo zinajumuisha Shilingi 113,893,184,000 fedha za ndani na Shilingi 38,879,696,000 fedha za nje; Soma hotuba yote hapa, bofya.


Post a Comment

0 Comments